Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuMuzikiMuziki wa Taarabu

Muziki wa taarabu ni mtindo maarufu sana katika mwambao wa Tanzania wa Tanga, Unguja na Pemba na Mombasa, Kenya. Muziki huu una chimbuko lake kutoka bara Arab na bara Hindi. Inaaminika kuwa muziki huu ulianzishwa na Seyyid Barghash bin Said (1870 – 1888), wakati alipoalika kikundi cha taarabu kutoka Misri kupiga kwenye Kasri yake. Baadaye alimpeleka Mohamed Ibrahim nchini Misri kujifunza muziki huo na aliporudi alianzisha Zanzibar Taarab Orchestra.

Kadiri siku zilivyopita, muziki huu ulizidi kujipatia umaarufu katika mwambao, matokeo yake ulienea Afrika Mashariki kote. Hivi sasa kuna vikundi vya taarabu ya kisasa, kwa mfano Jahazi Modern Taarab, East African Melody, Five Stars na Babloom Modern Taarab.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-18 11:27:22
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page