Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiElimuElimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi

Utoaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu/siyo Rasmi ni kipengele muhimu cha Sera ya Elimu ya Serikali kupambana na umaskini, ujinga na maradhi. Inalenga kuhakikisha kuwa watoto waliyo nje ya shule, vyama na watu  wazima, hasa wasichana, wanawake na makundi mengine yasiyobahatika wanapata fursa za mafunzo bora ya msingi. Kupitia mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu isiyo Rasmi, Wizara ilitayarisha Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) na Mpango wa Elimu ya Msingi kwa waliyoikosa (MEMKWA)

Katika kutekeleza MUKEJA na MEMKWA, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ilianzisha program ya kujua kusoma, kuandika na kuhesabu ya Ndiyo, Naweza pamoja na Vipindi vya Redio Kuimarisha Elimu (RISE). Programu ya "Ndiyo, Naweza", inalenga kutoa stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu na maarifa kuhusu mazingira yake ya kijamii – kiuchumi kwa vijana na watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu. RISE, iliyo sawa na MEMKWA, imelengwa kutoa elimu ya msingi kwa vijana na watoto waliyo nje ya shule wasioandikishwa katika shule za msingi rasmi, hasa kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi, wakiwemo wafugaji, jamii zinazohama hama. Kwa maelezo zaidi fungua, tovuti ya Ministry of Education and Vocation Training.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-24 16:54:44
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page