Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMawasilianoTeknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Teknolojia za Habari na Mawasiliano  zimepiga hatua tangu mwisho wa karne ya 20 na kusababisha kukutana kwa maudhui, ukokotoaji, mawasiliano ya simu na utangazaji. Teknolojia hizo zimeleta mabadiliko ika maeneo mengine pia hasa usimamizi wa maarifa na maendelo ya rasilimali watu. Ongezeko la uwezo wa TEHAMA umewezeshwa zaidi na  ukuaji wa mtandao wa kimataifa wa mitandao ya kompyuta inayojulikana kama intaneti. Imeathiri namna biashara inavyoendeshwa, imewezesha kujifunza na kushirikiana maarifa imesababisha imesababisha mtiririko wa maarifa duniani,  imewezesha wananchi na jamii kwa namna iliyosaidia  kuufafanua upya utawala bora na imeweza kuleta utajiri mkubwa na ukuaji wa kiuchumi na kusababisha kuwepo kwa jamii ya habari duniani.

Hivi sasa sekta ya TEHAMA nchini Tanzania imekuwa  huria na ushindani umeongezeka katika huduma ya simu za mkononi, idhaa za redio, huduma za intaneti na huduma za mawasiliano ya data. Chanzo kingine kipya cha mapato ni utumaji fedha kwa njia ya simu na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi. Kutandikwa kwa mkongo wa kimataifa nchini katika mwaka 2009 hadi 2010 kumeleta manufaa makubwa ya soko ambalo kabla ya hapo ilitegemea zaidi kuunganishwa na satelaiti zilizo ghali zaidi. Wakati huo huo Serikali imeanza awamu ya tatu ya mtandao wa taifa kuunganisha vituo vya wananchi nchi nzima.

Sera ya taifa ya TEHAMA imetaja maeneo kumi ya kuzingatiwa katika matumizi ya TEHAMA nchini Tanzania yanayojumuisha uongozi wa TEHAMA wa kimkakati; miundombinu ya TEHAMA; tasnia ya TEHAMA; mfumo wa usimamizi na sheria na rasilimali-watu; sekta za uzalishaji; sekta za huduma; utumishi wa umma; maudhui ya wenyewe na ufikiaji wa kimataifa. Kwa kifupi Sera ya ICT inaakisi malengo , madhumuni na matarajio ya kitaifa kama yalivyoelezwa katika Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 ikiwemo kuweka fursha za digitali ambazo Tanzania inaweza kuzitumia ili kufikia malengo ya dira hiyo mwaka 2025.

 

 

Miradi ya Taifa ya TEHAMA Machapisho na Tafiti za TEHAMA
Sera ya Taifa ya TEHAMA Miundombinu ya TEHAMA
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-26 11:27:22
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page