Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiSheria na TaratibuMsaada wa Kisheria

Nchini Tanzania, Msaada wa Sheria  hutoa ushauri wa bure kuhusu sheria na desturi inayosaidia masuala ya sheria kwa watu maskini, wasiomudu kulipia huduma za wakili. Msaada wa sheria ni pamoja na ushauri wa sheria, msaada, uwakilishi, elimu na taratibu za njia mbadala ya kusuluhisha mgogoro pamoja na wadau mbalimbali, kama vile mashirika yasiyo ya kiserikali, vyombo vya kitaaluma na taasisi za kitaaluma. Msaada wa sheria unaotolewa unatofautiana kwa mteja mmoja hadi mwingine kulingana na kesi inayohusika na mawakili  wanasaidiwa na vituo vya msaada wa sheria  vinavyoendeshwa na asasi za kiraia  vilivyoteuliwa pamoja na vyuo vikuu. Kushindwa kufanya hivyo inachukuliwa kuwa ni kuwanyima watu hao kupata haki kwa sababu msaada wa sheria  ndiyo msingi wa kufurahia haki nyingine, zikiwemo haki za kushtakiwa uonevu pamoja na kinga muhimu ya kuhakikisha utendaji wa haki wa msingi na imani ya wananchi katika mchakato wa haki.

Huduma za sheria zinazotolewa ni pamoja na ushauri na usahili, msaada wa kisheria kwa mtu mmoja mmoja ili waweze kujiwakilisha mahakamani, uwakilishi wa sheria mahakamani, ambapo mawakili wanawawakilisha wateja walioteuliwa, kuwezesha upatanishi na usuluhishi, kusaidia utayarisho wa nyaraka za kisheria KIV. Kuandika usia, mikataba, kuandika barua kwa viongozi, kujaza nyaraka za mahakama muhimu kwa kuanzisha mashauri, kusaidia kujaza maombi ya nyaraka nyingine katika mahakama au baraza la usuluhishi, kufuatilia masuala ya kisheria kwa asasi au watu kama vile Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kampuni na wizara, ufuatiliaji wa ufumbuzi wa mahakama, kama vile, rufaa, mapitio na upitiaji upya, uendeshaji madai ya kimkakati na ya maslahi ya wananchi na kutekeleza amri au maagizo. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Ministry of Constitutional and Legal Affairs

Huduma za Msaada wa Sheria za Vyuo Vikuu Chama cha Sheria ya Tanganyika (TLS)
Msaada wa Sheria kwa Simu Vigezo stahiki
Chuo cha Sheria Tanzania
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-27 12:14:08
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page