Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMawasilianoMtandao

Sekta ya Intaneti Tanzania haijaendelezwa kutokana na upungufu wa mtandao wa simu za kawaida  na ukosefu wa viungo vya mkongo wa kimataifa. Mpaka ulipoingia mkongo wa kwanza   wa kimataifa uliopita baharini mwezi Julai 2009, nchi ilitegemea zaidi viungo vya satelaiti kwa mtandao wa kimataifa wa intaneti, uliyosababisha  gharama kubwa za rejareja zilizoshindikana kumudu kwa  wananchi wengi.  Viduka vya huduma za intaneti vimechangia kwa kiasi kikubwa matumizi ya intaneti, lakini kuhusu kupenya kwa intaneti  nchini Tanzania bado kuko nyuma kuliko nchi nyingine katika kanda zenye viwango sawa vya pato la taifa na pato la kila mwananchi na kujua kusoma na kuandika.

Waendeshaji wa mitando ya simu za mkononi wana nafasi kubwa ya kuwa wachangiaji wakubwa wa huduma za intaneti kutokana na miundombinu mikubwa ya kitaifa, baada ya kuingia kwa huduma za data za simu za mkononi na 3G broadband. Mtindo mpya wa utoaji leseni umesababisha kuingia kwa  idadi kubwa ya watoa huduma kwenye soko.

Kuruhusiwa kwa itifaki  ya sauti kwenye intaneti (VOIP) pamoja na uanzishaji wa kizazi cha tatu na cha nne (3G,4G) cha simu za mkononi na mitandao ya siwaya inakuza sekta ya intaneti iliyokwazwa na kiwango cha chini cha maendeleo ya mtandao wa zamani wa simu za kawaida.

Kutokana na kuzinduliwa kwa huduma za simu za mkononi za 3G mobile broadband, mitandao ya simu za mkononi inazidi kuongoza katika watoa huduma za intaneti kwa kutumia muundombinu wa taifa ulioenea na wateja wengi waliopo katika soko la simu za kuongea.  Kunahitajika mapato zaidi kutoka kwenye huduma za data katika takribani mazingira yote ya kulipia kabla na kushuka haraka kwa ARPU sauti.  Chanzo kingine kipya cha mapato ni  uhamishaji wa fedha kwa njia ya simu ya mkononi na uwekaji fedha benki kwa njia ya simu.

 

Watoa huduma za mitandao
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-30 06:46:46
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page