Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMawasilianoUtafiti na Maendeleo

Mchango wa utafiti katika maendeleo hauna kifani. Lengo kuu la utafiti ni kuwa kama zana ya kuboreshea viwango vya maisha ya wananchi kwa kuchochea ukuaji na kuongeza tija katika sekta muhimu za uzalishaji za uchumi wa taifa. Katika ngazi ya makampuni, utafiti unaweza kuleta ubunifu wa bidhaa, uboreshaji wa bidhaa, kuongeza ufanisi wa huduma, tija na ubora wa utendaji katika soko.

Sera zinazoongoza utafiti zina mchango mkubwa katika kupanga maendeleo ya kiuchumi ya taifa. Sera hizi zimekuwa zikibadilika mara kwa mara ili kukidhi mahitaji ya jamii. Kimsingi sera hizi zimepitia vipindi vitatu. Katika kipindi cha miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970 ilikuwa kipindi cha sera ya sayansi, hali ya kuwa miaka ya 1970 na 1980 kilikuwa kipindi cha sera ya sayansi na teknolojia. Miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000 ni kipindi cha sayansi, teknolojia na ubunifu. Tofauti na vipindi viwili vya kwanza, kipindi cha tatu kinasisitiza zaidi nafasi ya sayansi katika maendeleo ya taifa na kinashirikisha kwa ukamilifu utafiti katika Dira ya Maendeleo ya Taifa na mikakati ya utekelezaji. Hatua hii   inahakikisha kuwa maarifa ya sayansi na teknolojia yaliyopatikana katika taasisi za utafiti yanakidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya taifa.

Historia inaonyesha kuwa nchi zilizozingatia sera zenye mwelekeo wa utafiti thabiti zimefanikiwa kujenga uchumi wenye ushindani. Bila shaka miongoni mwa sababu za mafanikio madogo ya kiuchumi ya nchi nyingi zinazoendelea licha ya kujaliwa kuwa na maliasili nyingi ni kushindwa kwao kutunga na kutekeleza sera za utafiti na maendeleo madhubuti kwa upande mmoja na kushindwa kwao kutumia matokeo ya utafiti kuendelezea rasilimali zao kwa kuboresha maisha yao kwa upande mwingine. 

Taasisi za Utafiti na Maendeleo Mamlaka ya kutafiti
Ruzuku za Utafiti Masijala ya Taifa ya utafiti
Miradi na Machapisho ya tafiti Sera ya Taifa ya Utafiti na Maendeleo ya mwaka 2010
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-30 08:20:18
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page