Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMawasilianoMawasiliano ya Simu

Tanzania ina sekta ya mawasiliano ya simu iliyo na ushindani kamili. Kuna kampuni mbili za simu za mezani na saba za mitandao ya simu za mkononi na kampuni nyingine nne zilizopewa leseni. Kampuni za simu za mezani ni TTCL na Zantel. Kampuni hizi hutoa pia huduma za simu za mkononi kitaifa na kimataifa. Mtandao wa TTCL umekuwa digitali tangu 2004. Hata hivyo idadi ya simu za mezani imeendelea kuwa ndogo. Wako wateja 300,000 tu na nyingi ya simu zao huwa hazifanyi kazi. TTCL pia inatoa huduma za ISDN yenye Basic  Rate Interface, Primary Rate Interface na huduma za ADLA broadband.

 Hadi Julai 2009, TTCL iliendesha mtandao wa IP nchi nzima kwa ajili ya kuunganishwa kitaifa na kimataifa katika intaneti, kwa kutumia mkongo wa digitali wa microwave 140Mb ili kuongeza viunganisho vya intaneti na CDMA wireless kufikia huduma za simu za mezani. Wizara ya Uchumi imeeleza mchango wa sekta ya mawasiliano katika pato la taifa 2007 kuwa ni zaidi ya asilimia 20.1. Aidha kwa mujibu wa TCRA wingi wa simu ni kipimo kuwa upataji wa simu na huduma nyingine za TEHAMA kwa watu 100 wanaoishi katika eneo maalum au kanda kimeongezeka. Kwa mfano mwaka 2000 wingi wa simu ulikuwa asilimia 1 tu lakini hadi Juni 2008 ilishapanda hadi asilimia 25, na mwishoni mwa 2009 ilifikia asilimia 43. Tanzania ni miongoni mwa masoko ya TEHAMA yanayokua kwa haraka sana barani Afrika. Hata hivyo ukuaji huu mkubwa  yabidi uchukuliwe kwa tahadhari kwani unategemea zaidi data ya watumiaji inayotolewa na kampuni za simu. Tahadhari katika kutafsiri data za matumizi ya simu inahitajika kutokana na sababu zifuatazo:

  • Wamiliki wengi wa simu wanaishi mijini, kwa hiyo kama ukokotoaji wa wingi wa simu utazingatia eneo la ardhi kama kigezo, takwimu za hapo juu zitapungua sana.
  • Simu moja inaweza ikatumiwa na kaya au kutumiwa na watu wengi mahali pa kazi
Uhamishaji wa Namba za simu za Viganjani Makampuni ya Simu yaliyosajiliwa
Watoa huduma za Mawasiliano Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-01 18:28:16
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page