Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMawasilianoSayansi, Teknolojia na Ubunifu

Siku hizi teknolojia imekuwa rasilimali muhimu ya maendeleo na chanzo cha ushindani wa sekta ya uzalishaji na sekta ya huduma. Kuna njia mbili za kupata teknolojia inayohitajika, ama kupitia ubunifu au uhawilishaji wa teknolojia.  Upataji wa teknolojia kupitia ubunifu na ugunduzi inahitaji kuelekezwa ili kupata manufaa makubwa zaidi kutokana na teknolojia hizo, kwa hiyo inahitajika mwongozo.

Maendeleo katika sayansi na teknolojia hutegemea zaidi namna uvumbuzi wa kiteknolojia unavyoendelezwa na kutumiwa. Serikali imetunga Sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia inayotaka kuanzisha utaratibu wa kutambua, kukuza na kuendeleza vipaji maalum katika sayansi na teknolojia miongoni mwa Watanzania, hasa vijana ili kunufaika na uwezo mkubwa wa kitaaluma  wa binadamu  unaohitajika kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Serikali imesisitiza kuhusu kumahasisha na kukuza utamaduni wa sayansi na  ubunifu wa kiteknolojia katika jamii.

Kuna umuhimu mkubwa wa kuunda miongozo na program za kubainisha, kutambua, kuendeleza na kukuza  wabunifu na wavumbuzi wazalendo nchini ili kuhimiza ubunifu na uvumbuzi katika jamii ya Tanzania. Miongozo hii imezingatia uchambuzi wa hali halisi ya huduma za teknolojia nchini Tanzania, mamlaka ya taasisi za serikali na zisizo za serikali zinazohusika na haja ya kuendeleza na kutumia uwezo wa ubunifu na uvumbuzi wa Watanzania. 

Miradi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Sera ya Sayansi na Teknolojia (S&T Policy, 1996)
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-01 19:15:02
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page