Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliUlinzi na UsalamaJeshi la Wananchi Tanzania - JWTZ

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania liliundwa Septemba 1964. Tangu kuzaliwa lilijengwa kwa vikosi ambavyo ni jeshi la wananchi chini ya udhibiti wa raia. Daima lilikuwa likikumbushwa tofauti yao na majeshi ya kikoloni. Walipewa dhima iliyodhahiri, kuilinda Tanzania na kila kitu cha Tanzania hasa watu na itikadi yao ya siasa. Jitihada kubwa zilifanywa katika mafunzo, kwa kutumia takribani robo ya muda wa mafunzo kwa ajili ya siasa. Matokeo yake ni kwamba si makamanda peke yao, bali wanajeshi wote walijua kwa uhakika nafasi zao kuhusiana na chama, serikali na wananchi.

Rais alikuwa mtendaji, pia mwenyekiti wa chama, msemaji mkuu wa sera za Taifa, falsafa ya siasa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania. JWTZ kama taasisi ilijua kwamba wapo kwa ajili ya rais, Serikali na chama. Aidha uteuzi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hadi makamanda wa vikosi ulikuwa ama unafanywa moja kwa moja na rais au idhini yake ilitakiwa. Mchanganyiko wa kijamii wa JWTZ ulitoa mchango mkubwa sana ndani ya Jeshi na baina ya Jeshi na jamii. Imeelezwa kwamba wanajeshi walitoka kwenye makabila mbalimbali. Pia walitoka kwenye tabaka zote za jamii. Maofisa walichaguliwa baada ya mafunzo ya jumla na si kutoka kwenye kundi maalumu na uteuzi wa komisheni ulitegemea utendaji wa mtu binafsi.Sehemu hii inakupa taarifa kuhusu JWTZ, muundo wake, historia, dhima na majukumu ya Jeshi hilo. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya JWTZ

Muundo wa JWTZ Kamandi ya Nchi Kavu
Kamandi ya Wanamaji Kamandi ya Anga
Historia ya Jeshi Dhima na Wajibu wa JWTZ
Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi Waliopita
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-12 16:07:58
Kufaa
4.3
6 Jumla
Inafaa Sana 4
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.2
5 Jumla
Rahisi Sana 4
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 1

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page