Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliUlinzi na UsalamaJeshi la Magereza

Jeshi la Magereza (TPS) lilianzishwa rasmi kama Idara Kamili ya Serikali tarehe 25 Agosti 1931. Kabla ya terehe hiyo, Jeshi hilo lilikuwa likifanya kazi chini ya Jeshi la Polisi. Mabadiliko haya hayakuleta uboreshaji zaidi wa hali ya Magereza kwa sababu mkazo ulibaki katika kufunga kwa usalama. Kuwafungia wafungwa katika Magereza yenye ulinzi wa hali ya juu yaliyojengwa katika miji mikuu na miji ya wilaya, kazi ngumu, na kubaguliwa kwa rangi, ilikuwa  sifa kubwa ya hali halisi ya Magereza. Sera hii ya Magereza ilikuwa ikiakisi msingi wake wa kifalsafa wa adhabu na kuondolewa uwezo ambayo imeendelea kuenea ingawa enzi ya ukoloni wa Kijerumani iliisha mwaka 1919. Utawala wa kiulinzi wa Uingereza uliisha kwa kupata uhuru mwaka 1961.

Baada ya uhuru, Sera mpya ya Magereza ilitayarishwa na kutumika kwa kuzingatia kuwatendea ubinadamu na haki wafungwa kuwa ni Maadili Makuu ya Sera. Madhumuni yalikuwa urekebishaji wa wahalifu kama mchango kwa usalama wa jamii. Kwa vitendo, mabadiliko haya ya mwelekeo wa kifalsafa yalidhihirishwa kwa kutunga Sheria ya Magereza ya 1967 inayozingatia zaidi nia ya Sheria za Kimataifa za kujali haki za msingi za binadamu kwa; kuanzisha Magereza ya Mashamba ya Wazi katika maeneo ya vijijini yaliyoteuliwa yawe vituo vya umahiri kwa kuelimishia stadi za kilimo kwa wafungwa na kueneza huduma hiyo kwa jamii zinazozunguka; kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi katika mikoa ya Mbeya na Morogoro kwa mafunzo ya stadi kwa wafungwa. Mafunzo haya yamehusishwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Taifa ili vyeti vya wahitimu vitambuliwe; kupanua miradi ya kiuchumi ndani ya Magereza ya Zamani yaliyorithiwa kwa ajili ya mafunzo ya stadi kwa wafungwa wa muda mrefu;k uanzisha program za elimu za ngazi mbalimbali katika Magereza, ikiwemo elimu ya msingi ya watu wazima, masomo ya kawaida ya elimu na elimu ya msingi kwa walioacha masomo katika Magereza ya Watoto na utumiaji wa mtaala mpya wa mafunzo kwa watumishi wa Magereza kwa kutumia mbinu mpya ya kufundishia itakayozingatia zaidi ufuataji wa haki za binadamu.

Kutokana na mwelekeo huo mpya, hali ya Magereza imeanza kubadilika na kuwa ya kujali ubinadamu na sifa na jina la TPS liliboreka ndani na nje ya nchi tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970.Hadi sasa TPS ina taasisi 122, ofisi za mikoa 21, Vyuo vya Mafunzo ya Watumishi viwili, Vituo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi vine na Makao Mkuu. Ofisi za mikoa zinatoa usimamizi wa kiutawala, hali ya kuwa Makao Makuu yanasimamia na kiutawala vituo vyote vya Magereza nchini.

Jeshi hili linalinda usalama wa umma kwa kuhakikisha kuwa wahukumiwa wote wanatumikia hukumu zao za kufungwa katika Magereza yanayozingatia ubinadamu, yasiyo na gharama na yaliyo salama zaidi. Jeshi hili linasaidia kupunguza uwezekano wa vitendo vya jinai baadaye kwa kuwashawishi wafungwa kushiriki kwenye program mbalimbali zilizothibitishwa kupunguza uhalifu sugu. Kwa taarifa zaidi tembelea Tovuti ya Jeshi la Magereza: www.magereza.go.tz


No Jeshi la Magereza Faili / Anuani Miliki
1 Orodha ya Magereza na Makambi yote Tanzania Bara 291.6 KB
2 Mawasiliano ya Jeshi la Magereza 302.4 KB
3 Mkataba wa Huduma Kwa Mteja 3.2 MB
Huduma kwa Wafungwa na Programu za Urekebishaji Magerezani Uhusiano Kimataifa
Maisha ya Gerezani Dira na Dhima ya Jeshi la Magereza
Majukumu na Malengo ya Jeshi la Magereza Muundo wa Jeshi la Magereza
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-13 06:00:00
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.5
2 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page