Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliUlinzi na Usalama Sera ya Ulinzi ya Taifa

Sera ya Ulinzi ya Taifa ni seti ndogo ya Sera ya Serikali inayohusika na kukabili vitisho vya kijeshi na maendeleo, utunzaji, matayarisho na ajira ya wanajeshi. Sera ya Ulinzi haiwezi kushughulikiwa peke yake, lakini inahitaji kutungwa kuwiana na vipengele vingine vya Sera ya Serikali, hasa Sera ya nje. Sera ya Ulinzi inahitaji kuwa na majeshi yenye kiwango cha juu cha tija ya jeshi, utayari wa kutosha, na kuwa na madhumuni yanayoeleweka kwa kuzuia migogoro, udhibiti wa migogoro, na shughuli za mapambano. Uwezo wa jeshi la ulinzi unakusudiwa kuwa wa chombo chenye uwezo mkubwa kupambana na uvamizi wowote, wakati wa amani na mgogoro. Sera ya Ulinzi wa Taifa kwa upande wake lazima ionyeshe maadili na maslahi ya taifa. Lengo la jumla la ulinzi wa taifa linazingatia kulinda maslahi na maadili makuu ya Taifa, yanayojumuisha kulinda uhuru wa taifa, dola na uadilifu wa taifa, kulinda Muungano, kudumisha amani na utulivu, kuhimiza demokrasia na utawala bora, kuhimiza ustawi wa kiuchumi na maendeleo ya uchumi na jamii, kudumisha amani na utengamano wa kanda, kudumisha haki katika jamii na kulinda maliasili.

Sera ya Ulinzi ya Taifa inasisitiza pia masuala muhimu yenye athari ya moja kwa moja ya usimamizi wa rasilimali watu, kama utayari wa jeshi, marekebisho ya kimuundo, watumishi wa kiraia, wanajeshi wa akiba, wa zamani na wastaafu na majeshi ya baadaye. Kwa taarifa zaidi soma Sera ya Ulinzi ya Mwaka 2004.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-14 13:00:54
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page