Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliUlinzi na Usalama Jeshi la Kujenga Taifa

Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa mwaka 1964 kwa Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuweka pamoja vijana wa Tanzania. Jeshi la kujenga taifa lilikusudiwa kwa vijana waliomaliza shule za msingi. Walifundishwa stadi zitakazowasaidia watakaporudi nyumbani, vijana walijitolea kwa miaka miwili, na mwisho wa mafunzo wengine walibaki katika jeshi hilo, walijiunga na jeshi, na waliajiriwa kwenye sekta za umma na za binafsi, hali ya kuwa waliowengi walirudi kwao wakiwa na stadi walizofundishwa walipokuwa Jeshi la Kujenga Taifa.

Mwaka 1966 Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa ilirekebishwa kujumuisha wahitimu wa kutoka elimu ya sekondari ya juu na taasisi za elimu ya juu kujiunga kwa lazima na kubaki kuwa hiari kwa watu waliomaliza elimu ya msingi na elimu ya sekondari. Jeshi la Kujenga Taifa limelenga kuwafanya wahitimu kutoka elimu ya sekondari ya juu na vyuo vya elimu ya juu, kulilipa taifa kwa kuwapa elimu. Ilikusudia  kuwachukua wanawake na wanaume vijana waliosoma kutoka kazi mbalimbali na kuwaunganisha kujenga hisia ya umoja wa kitaifa. eshi la Kujenga Taifa linachukua vijana kutoka mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya ubaguzi kwa misingi ya jinsia, dini au kabila. Lengo lake ni kuonyesha muundo wa jamii ya Tanzania. Zanzibar ina Jeshi la Kujenga Taifa lijulikanalo kama Jeshi la Kujenga Uchumi lililokusudiwa kukidhi mahitaji ya visiwa vya huko.

Watumiaji watapata taarifa kuhusu Jeshi la Kujenga Taifa, Chimbuko lake, Kazi na mafunzo mbalimbali inayoyatoa.

 

Kazi za Jeshi la Kujenga Taifa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-14 13:47:40
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page