Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliUlinzi na UsalamaMgambo

Wanamgambo inamaanisha kundi la watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaofanya kazi chini ya mamlaka au maelekezo ya serikali na wanaopata mafunzo ya kijeshi au wanaoshiriki katika mafunzo ya kijeshi na mazoezi ya kijeshi ya kusimamia utekelezaji wa sheria kwa ajili ya kulinda dola ya Jamhuri ya Muungano au kwa ajili ya kulinda watu au mali ya Jamhuri ya Muungano. Hii haijumuishi Jeshi la Polisi, sehemu yoyote ya Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa.

Mafunzo ya wanamgambo yalianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mgambo ya 1963 ya kulipatia jeshi raia wa Tanzania, wakulima na wafanyakazi waliotayari kulinda nchi yao kama moja ya sehemu za JWTZ. Azma ya Wanamgambo ni kujenga moyo wa uwajibikaji na kujivunia taifa kwa wananchi kwa kuwakaribisha wananchi kutoa mchango wao katika ulinzi wa nchi.

Serikali iliamua kuwashirikisha wananchi katika kulinda vijiji vyao. Kuanzishwa kwa wanamgambo kulikuwa pia kwa mujibu wa wazo la Rais Nyerere la kuwa na jeshi dogo la kitaalamu linalosaidiwa na wanamgambo wengi. Katika jamii za kiasili, kila mtu mwenye uwezo wa mwili usio na ulemavu, pia ni mwanajeshi, haja inapotokea. Kwa hiyo mfumo wa jeshi umetosheleza mahitaji ya ulinzi na usalama katika ngazi ya kijiji. Sehemu hii inakupa taarifa kuhusu Wajibu wa Mgambo na mafunzo ya Mgambo.

Wajibu wa Mgambo Mafunzo ya Mgambo
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-14 16:07:58
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page