Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliUlinzi na UsalamaJeshi la Polisi

Jeshi hili ni chombo cha muungano na kina mamlaka nchini Tanzania kote na kuundwa kwake huko kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Jeshi la Polisi limeundwa chini ya kifungu cha 3, cha sheria ya Jeshi la Polisi, Sura ya 322 ya Sheria za Tanzania kwa ajili ya kulinda amani, kuwapo kwa utawala wa sheria na ufuatiliaji wa utulivu, kuzuia na kubaini uhalifu, kuwakamata na kuwalinda wahalifu na kulinda mali ya nchini Tanzania. Jeshi linalenga kuhakikisha kuwapo kwa ulinzi na usalama wa watu na mali kupitia utunzaji wa amani, kuwapo kwa utawala wa sheria na ufuatiliaji wa utulivu, kuzuia na kubaini uhalifu, kuwakamata na kuwalinda wahalifu na kulinda mali ya Tanzania.

Dhima

Dhima ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama wa raia, ulinzi na kinga ya maisha na mali ya wakazi wote wa jamii yetu, kuratibu na kudhibiti mtiririko wa magari ili kuwezesha nyendo za watu na bidhaa ndani ya miji yetu na kupunguza athari ya uhalifu kwa wakazi wa jamii kupitia upelelezi, kukamata na kubaini watu waliohusika na makosa ya jinai.

Dira

Kuwa na polisi jamii wenye utaalamu, wa kisasa watakaosaidia utunzaji wa amani na utulivu kwa kupunguza matukio ya uhalifu na hofu ya uhalifu; kusimamia haki, utawala wa sheria na utawala bora na usalama wa raia nchini. Jeshi la Polisi lililorekebishwa lazima likubalike na kuaminika na jamii, kutambuliwa kutokana na  ushughulikiaji wake wa kitaalamu kwenye uhalifu na matukio katika matumizi ya vipaji vya kisasa, teknolojia na zana,

Maadili ya Msingi ni Utaalamu, Kutii maadili, Kumjali mteja, Uwajibikaji na utimizaji wajibu, Ushirikiano wa pamoja, Kutokuwa na upendeleo, Wajibu katika jamii, Uaminifu, Heshima, Utiifu, Utii wa Sheria na Kanuni, Kuwa tayari kutenda, Kujiamini na kutunza siri

Polisi Jamii Kazi za Jeshi la Polisi
Muundo wa Jeshi la Polisi
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-14 19:15:02
Kufaa
4.0
1 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page