Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiMalazi

Mahali pa kukaa nchini Tanzania

Malazi nchini Tanzania yanatofautiana, kuanzia nyumba za kitalu kwenye hifadhi za Taifa, majengo ya kale kwenye vichochoro vya Mji Mkongwe, nyumba za kupumzikia na mabanda kwenye fukwe zilizosambaa katika fukwe za Zanzibar, Dar es Salaam na maeneo yote ya pwani na hupungua gharama hadi kwenye hoteli yingi za kati na za bei rahisi mpaka nyumba za wageni za kawaida mitaani.

Kuna sehemu za aina nyingi za malazi zikiwemo Hoteli, Kambi, Sehemu za Kupumzika na Nyumba za kukaa familia.Maeneo ya kupiga kambi ya wazi yapo kwenye hifadhi za taifa nyingi. Baadhi zina vifaa na majengo yenye viwango vinavyokubalika kwa mfano mabomba ya maji, vyoo na  kuni, na mengine ni ya kawaida yenye eneo lililofyekwa kwa ajili ya kuegesha magari  na kupiga hema. Vibali vya kuweka kambi ya mahema ni lazima vilipwe pamoja na kiingilio kwa kila egesho. Unashauriwa kuulizia gharama na taratibu za mahali kabla ya kufika. Orodha ya maeneo ya kupiga kambi ya Serikali na ya binafsi inapatikana kwenye Hifadhi za Taifa Tanzania. (www. Tanzaniaparks.com).

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-23 20:48:34
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page