Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMajiHuduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini

Upataji wa maji safi na salama ni muhimu kwa kukabili umaskini na magonjwa yanayosababishwa na maji.  Zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanaoishi katika maeneo ya vijijini hawana maji safi kwa matumizi yao ya nyumbani, uzalishaji wa mazao na usafi wa kutosha.  Matukio ya magonjwa yanayosababishwa na maji, magonjwa yanayohusiana na maji, na magonjwa yanayoletwa na maji yanayosafiri yanaonyesha kuwa yameshamiri zaidi pale watu  wanapotumia maji yaliyosibika (machafu) au wenye uhaba wa maji kwa matumizi ya kila siku.  Wizara, kupitia Idara ya Maji vijijini inakusudia kuwa na upatikanaji maji endelevu vijijini kwa kuwapatia maji ya kutosha salama yanayoaminika kwa umbali usiozidi mita 400 kutoka kila kaya.

Miradi ya Maji vijijini inatekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mtaa kwa kushirikiana na wananchi pamoja na sekta bainafsi.  Sekretarieti za Mikoa zinafuatilia na kutoa msaada wa kiufundi.  Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI ina ratiba utekelezaji wa mradi wa maji.  Vijijini kwa upande mwingine, Wizara ya Maji inatafuta fedha za miradi hiyo na kutoa utaalamu na mwongozo kuhusu usimamizi wa maji

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-27 18:28:16
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page