Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiKodiUingizaji na Utoaji wa Bidhaa

Uingizaji bidhaa maana yake ni kuleta au kusababisha bidhaa kuletwa Tanzania kutoka nchi ya kigeni. Taratibu za uingizaji ni lazima zifuatwe ili kutoa bidhaa kutoka kwenye udhibiti wa Forodha kwa mujibu wa Kifungu cha 2(1) cha Sheria ya EACCMA ya 2004. Bidhaa zinazoingizwa Tanzania ni lazima zipitie hatua mbalimbali ambapo mtoaji wa bidhaa anashauriwa kujaza  nyaraka angalau siku saba kabla ya kufika kwa meli.

Utoaji wa bidhaa maana yake ni kuchukua au kusababisha bidhaa kuchukuliwa nje ya nchi. Bidhaa zinazosafirishwa nje huwa hazitozwi ushuru na kodi isipokuwa bidhaa za aina mbili: ngozi ghafi zinazotozwa asilimia 90 ya thamani ya FOB au shilingi 900 kwa kilo kutegemea kiwango gani ni kikubwa na korosho ghafi zinazotozwa kiwango cha asilimia 15 cha thamani ya FOB au $160 kwa tani ya metriki kutegemea ni kiwango gani ni kikubwa.

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya TRA.

Uwasilishaji wa Nyaraka Kabla Bidhaa Hazijafika Wakala wa Forodha
Utaratibu wa Usafirishaji Bidhaa Nje Viwango
Utaratibu wa uingizaji wa bidhaa
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-02 20:01:48
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page