Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMakaziMiliki Nyumba Yako Leo

Unaweza kumiliki nyumba yak oleo kwa kufuata taratibu rahisi za kuchukua fomu ya maombi kutoka kwenye ofisi yoyote ya NHC nchini kote (gharama ni sh. 2500) au kupakua kwenye tovuti ya NHC (Fomu ya Maombi) bure. Wasilisha fomu ya maombi iliyojazwa na uthibitisho wa amana ya 10% ya thamani ya nyumba (pamoja na VAT) kama ahadi ya kununua. Halafu maombi yako yatapitiwa kuhakikisha kutimiza kanuni na masharti ya NHC na kanuni za utwaaji wa nyumba za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama umefanikiwa, utapokea barua ya kupewa nyumba. Barua hii hupewa kwa mfuatano wa utumaji maombi, kwa wale wanaotimiza masharti yanayotakiwa. Halafu utatakiwa kulipa kiasi kilichobaki cha 90% ya thamani ya nyumba ndani ya muda wa siku 90 tangu tarehe uliyopewa. Iwapo uthibitisho wa mpango wa malipo hautalipwa ndani ya muda wa siku 90  zinazotakiwa NHC itawapa nyumba zilozotengwa waombaji wa kwenye orodha ya kusubiri. Iwapo malipo kamili hayatatolewa kulingana na tarehe za kulipa, au hukufanikiwa katika kipindi cha kusubiri, utarudishiwa 10% yako au kutumika kuombea nyumba nyingine ya NHC. Mauzo ya nyumba yatakuwa yamefungwa iwapo waombaji wote waliofanikiwa watalipa fedha iliyobaki na NHC itashughulikia hati miliki na kuzikabidhi kwa wanunuzi waliolipia fedha kamili, au kwa taasisi za fedha zinazohusika.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-11 07:33:32
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page