Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMakaziMpango Mkakati wa NHC 2010/11 - 2014/15

Shirika la Nyumba la Taifa la sasa liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 2 ya Mwaka 1990 ili kuendeleza kazi ya kujenga au kuwezesha ujenzi wa nyumba na majengo mengine nchini. Sheria hii ilifanyiwa marekebisho kwa Sheria ya Bunge Namba 2 ya Mwaka 2005 ambapo Shirika la Nyumba liliwezeshwa kufanya shughuli zake kwa misingi ya kibiashara. Kwa bahati mbaya katika hali yake ya sasa, Shirika limeshindwa kukabiliana na upungufu mkubwa wa nyumba uliopo nchini. Mpango Mkakati wa miaka mitano (2010/11 hadi 2014/15) umetayarishwa wakati huu ambapo serikali imedhamiria kushughulikia upungufu wa nyumba za makazi nchini. Hii inatokana na ukweli kwamba sekta ya nyumba inao uwezo wa kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi, kwa njia ya kuongeza mitaji, ajira mbalimbali, pamoja na kodi.

Mpango huu unaelezea dira, dhima, maadili ya msingi, malengo na matarajio ya Shirika. Pia mpango unaweka mikakati itakayotekelezwa ili kuliwezesha Shirika kujenga nyumba zisizopungua 15,000 katika kipindi cha utekelezaji wa mpango. Wakati wa utekelezaji wa mpango huu, Shirika litaelekeza nguvu zake katika kujenga uwezo, kutumia rasilimali zake kikamilifu na kuzingatia mahitaji kwenye soko la nyumba. Aidha, Shirika litajenga uhusiano na wadau wengine katika sekta ya nyumba kama vile Serikali, taasisi za fedha na watoa huduma za miundombinu (barabara, maji, umeme n.k). Mpango huu ambao umetayarishwa kwa njia shirikishi unalenga kulibadilisha Shirika ili liwe Shirika kiongozi katika masuala ya ujenzi. Ili kufikia lengo hili, Shirika litaundwa upya kuliwezesha kuboresha utendaji wake na hivyo kuboresha taswira yake. Hivyo basi, menejimenti ya Shirika inawajibika kwa kutelekeza malengo yaliyowekwa kwenye mpango huu. Naamini kuwa kujituma, ushirikiano na weledi wa wafanyakazi kutaliwezesha Shirika kufikia malengo yake yote yaliyoanishwa kwenye mpango huu.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-12 16:07:58
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page