Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba Vibali
OFISI INAYOHUSIKA
Uhamiaji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Watu wote wanaokusudia kuishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa biashara au kazi au madhumuni mengine yoyote yanayokubaliwa wanapewa vibali vya ukazi. Kibali cha daraja B kinakusudiwa kwa waombaji wenye sifa adimu au stadi, hasa kwenye kazi ya teknolojjia ya juu sana; ambazo wataalam wake hawapatikani kwa urahisi katika soko la ajira la hapa nchini.

Masharti:

 • Barua ya maelezo ya ziada inayoambatishwa au barua ya ajira.
 • Picha tano, wasifu, sifa ya elimu na maelezo ya majukumu ya kazi.
 • Muundo wa kampuni.
 • Barua ya ruhusa kutoka Serikalini.
 • Vyeti vya wanachama au ruhusa kutoka taasisi za kitaaluma za nchini
  kwa ajili mya kupima na kufuatilia  uadilifu wa kitaaluma wa wataalamu wa kigeni.
 • Nakala za kurasa za pasipoti.
 • Uthibitisho (nakala) za matangazo ya nafasi za kazi pamoja na wasifu wa Mtanzania mbadala.

 Taratibu:

 • Kamilisha/ Jaza Fomu ya Uhamiaji Tanzania bure na bila ada ya kushughulikia.
 • Wasilisha fomu kwa Kamishna  wa kazi kwa ajili ya mapendekezo.
 • Mapendekezo yataambatishwa kwenye fomu na kupelekwa kwa mkurugenzi wa uhamiaji kwa hatua zaidi.
 • Kamishna wa kazi anapitia maombi na kutoa mapendekezo ya kukubali au kukataa kwa idara ya uhamiaji.
 •  Pata kibali cha  Daraja B.

Zingatia:

 • Wageni wanaokusudia kufanya baadhi ya kazi za muda mfupi wataweza
  kusamehewa masharti  ya kupata mapendekezo ya Kamishna wa kazi mfano
  ni pamoja na wasanii, waburudishaji, waandishi wa habari, wawindaji nk.
  Vibali vya muda mfupi huamuliwa na Mkurugenzi wa Uhamiaji.

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 20-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page