Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba Vibali
OFISI INAYOHUSIKA
Uhamiaji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Mgeni yeyote anayetaka kukaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji, biashara, ajira au shughuli nyingine yoyote halali anaweza kupewa kibali cha ukazi. Utoaji wa kibali cha Ukazi uko kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Nam. 7 ya Mwaka 1995 na kanuni za mwaka 1997.

Vibali vya Daraja A:

Kibali cha ukazi cha daraja A kinaweza kupewa mtu zaidi ya mhamiaji aliyepigwa marufuku, anayekusudia kuingia au kubaki nchini Tanzania na kujishughulisha na biashara, utaalamu, kilimo, ufugaji, utafutaji wa madini au utengenezaji.

Masharti:

 • Cheti cha umahiri kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania (T.I.C)
 • Barua ya maelezo iliyoambatishwa.
 • Picha sita na wasifu.
 • Vyeti vya elimu (kama vinafaa) na cheti cha hisa (kama kinahitajika)
 • Usajili wa kampuni, katiba na kanuni za kampuni
 • Uthibitisho wa maeneo ya biashara
 • Uthibitisho wa sekta ya wizara yoyote inayohusika
 • Nakala ya kurasa za pasipoti zinazothibitisha uraia wa muda wa kutumika kwa pasipoti
 • Vyeti vya usajili kutoka mamlaka za usimamizi zinazohusika (Biashara nyingine zinahitaji idhini ya mamlaka mahususi za usimamizi);
 • Cheti cha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) (Kwa biashara zinazostahili kulipa kodi ya aina hii)
 • Cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (T.I.N)
 • Leseni ya biashara na hati ya udhibitisho wa kodi
 • Hati ya vivutio (kwa biashara zilizosajiliwa T.I.C au ZIPA kwa Zanzibar.
 • Uhawilishaji wa Hisa/ Hati ya Hisa (iwapo mwombaji ni mwenye hisa kutokana na baadhi ya hisa kuwahilishwa kwake)
 • Uamuzi wa bodi K.V udondozi wa mkutano wa bodi uliopitishwa kumteua
  mwombaji kuwa mkurugenzi (iwapo mwombaji hakuwa miongoni mwa
  wakurugenzi wa kwanza)
 • Faida ya mgao wa hisa (Fomu Nam.55(a)) kutoka kwa msajili wa kampuni iwapo
  mwombaji amegawiwa baadhi ya hisa na lazima uambatishwe uamuzi wa bodi
  uliopitishwa kupanua mtaji wa kampuni na kugawa kiasi Fulani cha hisa kwa
  mwombaji.


Taratibu:

 • Jaza Fomu ya Uhamiaji Nam.1, inayopatikana kwenye ofisi yoyote ya uhamiaji
 • Pata ushauri wa mamlaka ya usajili wa biashara na utoaji wa leseni kuhusu
  namna ya kusajili kampuni au biashara katika Jamhuri ya Muungano wa
  Tanzania
 • Udondozi kutoka kwa msajili kwa ajili ya biashara na si usajili kama kampuni ya
  Dhima yenye kikomo.
 • Onyesha leseni za biashara (leseni maalumu: leseni ya kawaida, leseni ya
  uchimbaji madini, leseni ya casino, leseni ya wakala wa huduma za utalii) n.k
 • Hati ya hisa (iwapo mwombaji ni mwenye hisa katika kampuni iliyosajiliwa)
 • Lipa ada kama ilivyo onyeshwa kwenye jedwali la Malipo.
 • Idhini haitaendelea kutumika baada ya siku 60 kuanzia tarehe ya taarifa
  kama hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 29 ya Kanuni za Uhamiaji, za mwaka 1997.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 20-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page