Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba PasiPoti/Pasi/Visa
OFISI INAYOHUSIKA
Uhamiaji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Inatolewa kwa mgeni, Isipokuwa mhamiaji aliyepigwa marufuku, ambaye ni mtegemezi halali wa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au mgeni mwenye kibali halali baada ya kuombwa na watu hao.

Masharti:

 • Mtegemezi ni lazima awe mke, mtoto au ndugu/jamaa wa mwombaji
 • Aweze kutoa malazi ya kutosha kwa mtegemezi huyo
 • Ni lazima uhakikishe kipato cha kutosha kumwezesha kumhudumia kwa ukamilifu mtegemezi huyo.
 • Ni lazima awe raia wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania au mgeni yeyote anayeishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye kibali halali
 • Picha sita za pasipoti

Taratibu:

 • Jaza Fomu ya Maombi
 • Ambatisha nakala ya pasipoti ya mtegemezi iliyohalali kutumika si chini ya mwaka mmoja
 • Wasilisha pasipoti halali (kwa ajili ya wote)
 • Toa kibali halali cha ukazi
 • Wasilisha uthibitisho wa uhusiano wa mwombaji na mtegemezi
 • Uthibitisho wa uwezo wa mwombaji kutoa makazi na namna ya kujikimu
 • Ambatisha picha. 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 20-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page