Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba PasiPoti/Pasi/Visa
OFISI INAYOHUSIKA
Uhamiaji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Visa ni idhini inayotolewa kwa mgeni zaidi ya mhamiaji aliyepigwa marufuku kuingia na kubaki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya matembezi, biashari matibabu, masomo au shuhuli nyingine zozote zinazotambulika kisheria. Zaidi ya hayo viza inaweza kupatikana kwenye ubalozi  wowote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Ubalozi Mdogo na pia baada ya kuwasili kwenye vituo vya kuingilia nchini.

Masharti:

 • Pasipoti au hati ya kusafiria inayotambuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 • Kibali cha ukazi au pasi inatolewa kwa mujibu wa Sheria ya uhamiaji Na. 7 ya Mwaka 1995.
 • Viza halali (Hii ni kwa raia wa nchi zinazohitaji visa).
 • Picha tano za pasipoti
 • Nyaraka za kampuni au biashara itakayotembelewa( kwa viza ya kuingia mara nyingi)
 • Uthibitisho kwamba mwombaji anatakiwa kusafiri mara kwa mara kuja Jamhuri  ya
  Muungano wa Tanzania (viza ya kuingia mara nyingi)
 • Nakala ya pasipoti halali au kitambulisho kingine cha mtu wa kutembelewa(mwenyeji wa mwombaji kama inatakiwa)

 Taratibu:

 • Jaza Fomu ya Maombi.
 • Ambatisha dhamana iliyojazwa kwa ukamilifu(kw a viza ya kuinggia mara nyingi)
 • Wasilisha maombi kwenye ofisi ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Dar es salaam au
  kwenye ofisi ya kamishna wa uhamiaji  Zanzibar.
 • Lipa kiwango cha ada kinachotakiwa, visa ya kawaida Dola za marekani 50,kwa
  visa ya kuingia mara nyingi, Dola za Marekani 100 na kwa viza ya kupitia ni Dola 30.

Zingatia:

 • Kuwa na visa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitoi haki ya moja kwa moja
  kuingia nchini kwa aliyenayo.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 20-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page