Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kusajili
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Chakula na Dawa

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Chanjo ni utayarishaji wa kibaiolojia unaoboresha kinga ya ugonjwa mahususi. Kwa kawaida chanjo ina ajenti kinachofanana na kimelea kinachosababisha ugonjwa na mara nyingi hutengenezwa kutokana na au aina fulani au vijiumbe maradhi, sumu yake au miongoni mwa protini yake ya juu. Nchini Tanzania, Kifungu 51 (1),  Sheria ya Mwaka 2003, kinaipa mamlaka TFDA kusajili dawa zote, zikiwemo chanjo.

Masharti:

  • Bidhaa ni lazima iwe kwa maslahi ya umma
  • Lazima iwe salama, yenye kufaa na ubora unaokubalika
  • Majengo/maeneo na shughuli za uzalishaji ni lazima vikidhi masharti ya sasa ya GMP
  • Bidhaa ni lazima zikidhi masharti mengine yoyote yatakayoelezwa na mamlaka kuhusu data za sumu kabla ya tiba
  • Ni lazima ziwe na data za usalama wa kitiba na kufaa

Taratibu:

  • Wasilisha data kuhusu kemia, utengenezaji na ubora wa kinga maradhi
  • TFDA baada ya kutoa sababu kwa maandishi, inaweza kukataa, kuahirisha, kubatilisha au kufuta usajili wa chanjo au kurekebisha masharti ya usajili wake
  • Uhalali wa usajili ni miaka mitano
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page