Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kutoa Malalamiko
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Unyanyasaji wa mtoto kimwili, kingono, kiakili, kihisia, utesaji au kutelekezwa kwa mtoto au watoto. Licha ya hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa, watoto wengi bado hawapewi ulinzi unaofaa.

Masharti:

 • Mtoto anayenyanyaswa
 • Mfanyakazi anayepata tuhuma ya unyanyasaji kutoka kwa mtoto
 • Mtu anayeelewa au anashuku kuwa unyanyasaji unafanyika au umefanyika

Taratibu:

 • Toa taarifa haraka kwa meneja au mtu aliyeteuliwa, si zaidi ya saa 24
 • Jaza fomu CP 1
 • Iarifu polisi na toa taarifa kuhusu mtu ambaye amemdhuru mtoto, au amemuweka mtoto katika hatari kubwa ya kudhurika
 • Meneja atamteua mtumishi maalumu kufanya uchunguzi katika kipindi cha saa 24 au watamaliza uchunguzi wao wenyewe
 • Polisi au meneja atamhoji mtoto
 • Uchunguzi wa awali ni lazima ukamilike ndani ya siku saba
 • Meneja au mtumishi maalumu atatayarisha ripoti ya maandishi yenye maelezo ya hatua iliyopendekezwa ichukuliwe kumlinda mtoto au watoto
 • Wasilisha nakala ya ripoti kamili ya uchunguzi na mapendekezo kwa kamishna wa ustawi wa jamii
 • Meneja atatekeleza mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti, iwapo meneja anaamua kutotekeleza mapendekezo, ataandika ripoti nyingine zaidi kwa kamishna wa ustawi wa jamii katika kipindi cha siku 14 na kueleza sababu za kutotekeleza mapendekezo.
 • Kamishna atakuwa na mamlaka ya kumwamuru meneja baada ya kupokea ripoti iliyoandikwa kwa mujibu wa sheria, ama kutekeleza mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti au kutekeleza hatua mbadala itakayoelezwa kwa kina kwa maandishi
  na kupewa meneja

Zingatia:

 •   Iwapo malalamiko yanahusu meneja, mtumishi maalum aliyeteuliwa atawasilisha
    tuhuma kwa kamishna wa ustawi wa jamii, iwapo malalamiko yanamhusu mtu
    aliyeteuliwa, meneja atapeleka uchunguzi wa awali kwa kamishna wa ustawiChanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page