Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kutoa Malalamiko
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Utaratibu wa malalamiko unahusu hasa nyumba za kutunzia watoto lakini pia unahusu huduma zote za umma na AZISE kwa watoto na familia zao. Iwapo malalamiko yanahusu udhalilishaji mtoto kimwili, kingono, kiakili au kihisia, itabidi sera ya kumlinda mtoto wa taratibu za kumlinda mtoto zitumike. Miongozo hii inatolewa kwa mujibu wa sheria ya 49 ya sheria za nyumba za kutunzia watoto.

Masharti:

 • Mtu yeyote anaweza kulalamika

Taratibu:

 • Shirika linatakiwa kuchunguza malalamiko
 • Utaratibu wa malalamiko ni lazima uweze kushirikisha watoto na wazazi wao au walezi
 • Mfumo huo ni lazima uelezwe kwa wazazi na watoto, na lazima ueleweke kwa urahisi ikiwemo uwezekano wa kuwasiliana na kamati ya ustawi
 • Malalamiko ni lazima yachunguzwe na kutatuliwa haraka kadiri iwezekanavyo
 • Jibu la mwisho kwa malalamiko rasmi ni lazima litolewe kwa maandishi kwa mlalamikaji
 • Watoto ni lazima waelezwe kwa ukamilifu matokeo ya malalamiko kwa namna watakayoweza kuelewa

Zingatia:

 • Walalamikaji wote wana haki ya kukata rufaa dhidi ya matokeo ya uchunguzi wa malalamiko pale ambapo mlalamikaji hakuridhika
 • Watoto wasiadhibiwe kinidhamu au kuteswa kwa namna yoyote kutokana na kutoa malalamiko
 • Shauku ya mtoto itakuwa ni kuzingatiwa kwa utekelezaji wa utaratibu wa malalamiko na katika uamuzi wote uliochukuliwa
 • Vyombo vinavyohusika na kutekeleza utaratibu wa malalamiko, nyumba za kutunzia watoto, idara ya ustawi wa jamii, makao makuu (DSWHQ) na kamati ya
  ustawi 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page