Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Mapato Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Leseni ya udereva ni waraka rasmi unaoeleza kuwa mtu anaweza kuendesha chombo cha mota kama vile pikipiki, gari dogo, lori au basi, katika barabara ya umma. Aidha mtu haruhusiwi kuendesha gari ya daraja yoyote barabarani isipokuwa kama ana leseni halali ya udereva au leseni ya kujifunzia udereva aliyopewa kwa daraja hiyo ya gari.

Masharti na Kanuni:

  • Ni lazima uwe na umri wa zaidi ya miaka 18 kwa gari na miaka 16 kwa pikipiki
  • Cheti cha ustadi wa kuendesha gari kutoka NIT na VETA.

Taratibu:

  • Nenda kwenye Ofisi ya Usalama Barabarani ukiwa na leseni yako ya udereva ya zamani
  • Wasilisha cheti cha uwezo wa kuendesha
  • Eleza aina ya gari unayokusudia kuendesha
  • Lipa ada ya leseni ya udereva ya Tsh.40,000/= na Tsh.3,000/= za kujaribiwa. Ada ya leseni ya muda ya Tsh.10,000/=
  • Utapewa daraja ya leseni kulingana na ufanisi wako.

Zingatia:

  • Mtu yeyote anayemiliki au anayesimamia gari au trela ya kundi lolote hatamruhusu mtu yeyote kuendesha gari hilo isipokuwa kama mtu huyo ana leseni halali ya udereva au ya kujifunzia aliyopewa kulingana na daraja ya gari au tela.

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page