Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Maliasili na Utalii

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Mwendesha safari za kitalii anahusika na kupanga na kuongoza safari za kitalii kwa wasafiri wanaotaka maelekezo ya mtu anayefahamu kuwaongoza kwenye mahali penye vivutio.  Kwa kawaida hutoa maelezo kwa mdomo kuhusu maeneo na sehemu za kihistoria wakati mtu mwingine akiendesha gari inayosafirisha watalii.

 Masharti:

  • Kanuni za Kampuni iliyosajiliwa Tanzania.
  • Majengo ya ofisi kwa ajili ya kufanyia shughuli za safari za kitalii.
  • Kundi la magari yasiyopungua matano yenye uwezo wa kusafiri (si zaidi ya  miaka mitano kutumika)
  • Magari ya kitalii ni lazima yawe na kina kubwa.
  • Andika jina la mwendesha safari za kitalii kila upande wa gari.
  • Magari ya safari za kitalii ni lazima yaonyeshe waziwazi leseni ya Wakala wa safari za kitalii kwenye gari husika.

Taratibu

  • Jaza Fomu ya Maombi
  • Wasilisha cheti cha usajili na katiba
  • Lipa ada iliyoelezwa

 

Zingatia:

  • Vibandiko haviruhusiwi wakati wa kutafuta leseni.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page