Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kutoa Malalamiko
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Katiba na Sheria

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Iwapo mashtaka ya Dola kwa mtu au shirika, kwa kufanya kosa na kuhesabiwa kuwa ni hatia dhidi ya Dola. Mamlaka ya mahakama za mwanzo kuhusiana na maswala ya jinai ni kwa kesi zote isipokuwa mauaji, uhaini na mengine yanayosababisha kifungo cha muda usiozidi miezi 12 au faini isiyozidi Tsh.200000/= (laki mbili)

Taratibu:

 • Toa taarifa ya kosa kwenye kituo cha polisi cha karibu au fungua mashataka mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo
 • Baada ya kuridhika kuwa kuna uwezekano au sababu za kutosha, itatolewa amri ya kukamatwa
 • Mtuhumiwa ni lazima afikishwe mbele ya Hakimu wa Mahakama ya mwanzo
 • Mtuhumiwa na mlalamikaji ni wanatakiwa kuwasilisha ushahidi wao
 • Kesi inasikilizwa mbele ya si chini ya wazee wawili wa baraza
 • Uamuzi wa mahakama utatokana na wingi wa kura

Ukomo wa Hatua Kutekelezwa:

 • Wiki sita- kwa kurudisha maombi yaliyokataliwa kwa kukosa mashtaka
 • Miaka mitatu kwa madai ya fedha zilizokopeshwa au baki ya fedha kwa mali iliyouzwa
 • Miaka mitatu kwa madai ya kuvunja makubaliano ya mdomo.
 • Miaka 12 kwa maombi ya mashtaka ya agizo au amri ya mahakama
 • Miaka 6 kwa madai yanayotokana na uvunjaji wa mkataba wa maandishi zaidi ya masuala yanayohusiana na ndoa na talaka
 • Miaka mitatu kwa mashtaka kwa msingi wa kosa la kidaawa.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page