Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Huduma za posta, maana yake ni mfumo wa kukusanya, kupeleka, kuwasilisha, kuzuia na kuwasilisha barua na vifurushi kwa njia ya posta  au kupitia leseni ya posta ya umma.  Huduma ya usafirishaji barua na vifurushi maana yake huduma maalumu kwa ajili ya upokeaji haraka, uhawilishaji  na uwasilishaji vifurushi vya posta zaidi ya barua.

Masharti:

 • Nakala ya leseni ya biashara iliyothibitishwa.
 • Lazima usajiliwe na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa madhumuni ya kodi.
 • Cheti cha uandikishaji au usajili.
 • Kampuni iliyosajiliwa Tanzania na kumiliki angalau 35% nchini.
 • Mpango wa biashara kwa huduma iliyopendekezwa.
 • Mpango wa utekelezaji wa huduma-matarajio ya ubora wa malengo ya huduma.
 • Njia za kutosha za usafiri.

Taratibu

 • Lipia Tshs. 10,000/= zilizoelezwa na zisizorudishwa.
 • Jaza fomu ya maombi na rudisha kwa mamlaka.
 • Wakaguzi wa  TCRA kwenye maeneo/majengo ya waombaji kuhakiki yaliyomo kwenye fomu ya maombi.
 • Lipa ada ya leseni.
 • Wasilisha stakabadhi kwa mamlaka.
 • Mchakato wa leseni unatarajiwa kuchukua si zaidi ya siku 30.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 23-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page