Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Wakala ya Meli au Wakala wa Meli ni uteuzi wa mtu au wakala inayohusika na kushughulikia usafirishaji wa bidhaa na shehena katika bandari duniani kote kwa niaba ya kampuni za meli.

Masharti:

 • Kampuni iliyosajiliwa yenye hisa nyingi za wananchi wa Tanzania.
 • Eneo la ofisi lisilopungua mita za mraba 18.
 • Vifaa vya mawasiliano
 • Akaunti ya Benki
 • Mtaji usiopungua Dola za Marekani 10,000 au kiasi kinacholingana kwa Tshs. (Kampuni zinazomilikiwa na Watanzania).
 • Mtaji usiopungua Dola za Marekani 100,000 au kiasi kinacholingana kwa Tshs. (Kampuni zinazomiliki kuwa na watanzania na wageni).
 • Hakikisha uwiano wa uwezo wa kulipa madeni kubaki 2.1.
 • Kuwa na watumishi wenye sifa katika tasnia ya usafirishaji wa bidhaa kwa meli.
 • Makubaliano ya Wakala na mwajiri.

 

Taratibu:

 • Jaza Fomu ya Maombi kutoka ofisi za SUMATRA au pakua kutoka kwenye tovuti ya SUMATRA.
 • Wasilisha fomu zilizojazwa kwa ukamilifu kwenye ofisi za SUMATRA.
 • Ushughulikiaji na idhini.
 • Lipia ada Dola za Marekeani 20 au kiasi kinacholingana kwa Tshs.
 • Kabla ya kutolewa leseni, kutafanyika ukaguzi wa  kujua ofisi ilipo.
 • Lipa ada ya mwaka ya Dola za Marekani 2000 au kiasi kinacholingana kwa Tshs. kama idhini ya maombi.
 • Nakala ya leseni iliyopita (kwa kuongeza muda)
 • Nakala ya leseni ya biashara
 • Gharama/ushuru  kwa huduma iliyotolewa
 • Nakala ya makubaliano ya wakala ya meli/mkataba, taarifa ya benki kwa mwaka
  uliotangulia shughuli.
 • Makubaliano ya upangaji au uthibitisho wa umiliki wa majengo ya ofisi.
 • Orodha ya wasifu wa wafanyakazi wa Menejimenti.
 • Orodha ya wafanyakazi wote.
 • Hesabu za fedha zilizokaguliwa kwa mwaka uliopita.
 • Ada na kamisheni ya wakala inayolipwa na mwajiri kwa wakala kwa huduma
  zilizotolewa, na isiwe chini ya zile zilizotolewa  katika Kanuni za Wakala ya Meli
  (Kima cha Chini cha Ada ya Wakala na Kamisheni) za Mwaka 2011
  .
 • Nakala ya kurasa za pasipoti zinazoonyesha maelezo ya mwenye pasipoti/au cheti
  cha kuzaliwa/hati ya kiapo kuthibitisha uraia – kwa mgeni ni lazima kujumuisha
  kibali halali cha kazi.
 • Nakala ya katiba na kanuni za kampuni.
 • Mwanahisa wa kigeni ni lazima aonyeshe maelezo ya usajili wa kampuni.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page