Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Gari lolote lenye uwezo wa kuchukua watu saba na kuendelea linatakiwa kuomba leseni ya njia ya usafiri.  Mamlaka inatoa leseni za muda mfupi - hutumika kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu na  leseni za muda mrefu - hutumika kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Masharti:

Fomu za maombi zinatumwa katika nakala mbili pamoja na viambatisho vifuatavyo;

  • Kadi za usajili wa gari
  • Ripoti ya ukaguzi wa gari
  • Cheti cha bima halali na
  • Leseni iliyopita (kwa kuongeza muda)

 

Taratibu:

  • Jaza fomu zinazotakiwa
  • Lipa ada ya kushughulikia ya Tshs. 2,000/=
  • Lipa ada ya leseni inayotofautiana kulingana na ukubwa wa injini na muda wa leseni.
  • Wasilisha fomu kwenye ofisi ya SUMATRA iliyopo mkoani kwako.

 

Zingatia:

  • Njia ya usafiri, ratiba na nauli za basi zinategemea uthibitisho wa SUMATRA.

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page