Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kusajili
OFISI INAYOHUSIKA
Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji Leseni

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Jina la biashara ni jina ambalo mtu au vyombo vingine vya kisheria, huuzia biashara. Jina hilo si kama linakutambulisha wewe na wateja wako tu, hukuwezesha pia kutofautisha na washindani wako kuonyesha msisimko wa biashara yako. Kwa biashara nyingi, jina mara ni rasilimali ya thamani kubwa sana.

Masharti:

 • Mwombaji ni lazima sjaze fomu ya maombi ya kusajili jina la biashara:
  • Kwa mtu mmoja mmoja, jaza fomu namba 3
  • Kwa ubia, jaza fomu namba 2
  • Kwa shirika, jaza fomu namba 8.
 • BRELA hufanya utafutaji na uhakiki wa majina
 • Huthibitisha au kukataa ombi
 • Mwombaji hulipa ada zifuatazo:
  • Ada ya maombi y ash.5,000/=
  • Ada ya matunzo y ash. 1,000/= (hulipwa kila mwaka)
  • Ada ya utafutaji na uhakiki sh. 1,000/=
  • Mwombaji hupewa cheti na udondozi atakaotumia mwombajikufungulia akaunti.

Kubadili Jina La Biashara

 • Mwombaji anajaza fomu namba 6
 • Baada ya kulipa ada zinazostahili, cheti cha kubadili jina kinatolewa pamoja na udondozi mpya.

Kubatilisha Matumizi Ya Jina La Biashara

 • Mwombaji anajaza fomu Nam. BN7 (fomu ya kukoma/kuacha kwa muda)
 • Ataambatisha cheti cha usajili halisi
 • Atalipa ada ya kukoma/ kuacha kwa muda ya sh. 1,500/=

Zingatia:  Ada zote zilizotajwa zinaweza kupitiwa upya kila baada ya muda.

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page