Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji Leseni

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Sehemu ya utoaji leseni za viwanda inatekeleza sheria ya utoaji leseni na usajili wa viwanda Na. 10 ya 1967. Sheria hii inatoa fursa ya uendelezaji na uhamasishaji viwanda kuwezesha usajili na utoaji leseni za viwanda. Kuna njia mbili za kutoa leseni za viwanda kwa kampuni na inategemea iwapo kampuni inayoomba imepitia kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) au hapana.

Masharti

 • Nakala ya maelezo ya mradi
 • Nakala ya cheti cha jina la Biashara / cheti cha usajili.
 • Fomu ya maombi iliyojazwa kwa ukamilifu.
 • Ada ya maombi ya 800,000/=

Utaratibu

Maombi kupitia bodi ya utoaji leseni za uendeshaji viwanda:

Maombi yajumuishe nyaraka zifuatazo:

 • Nakala ya upekuzi yakinifu
 • Nakala ya cheti cha usajili
 • Fomu ya maombi iliyojazwa kwa ukamilifu.
 • Matayarisho ya makala ya bodi
 • Uwasilishaji wa maombi kwa bodi ya utoaji leseni za uendeshaji viwanda kwaajili ya uthibitishwaji / kukataliwa.

Maombi kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC)

 • Wasilisha nyaraka zifuatazo:
 • Nakala ya cheti cha motisha / vivutio vya TIC
 • Nakala ya upembuzi yakinifu.
 • Fomu ya maombi iliyojazwa kwa ukamilifu.

Zingatia: Fomu hizo zinapelekwa kwa msajili wa viwanda, BRELA.

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page