Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Wakala ya Uchimbaji na Ujenzi wa Visima

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Ujenzi wa Kisima cha Kina kirefu

Ujenzi wa Kisima cha Kina kirefu imesaidia kuongeza hali ya upatikanaji wa maji safi na salama  kwa matumizi ya nyumbani, umwagiliaji , matumizi ya viwandani nk. hali hii imesaidia kuboresha hali ya maisha ya Watanzania wengi. Visima vya kina kirefu vimejengwa na serikali, hasa katika maeneo ya vijijini ili kuakikisha kuwa watu wanapata maji safi na salama. Aidha visima vya kina kirefu vimejengwa kwa mashirika yasiyo ya serikali, wananchi, viwanda na watu binafsi.

Taratibu:

 • Tembelea ofisi ya maji ya Bonde karibu yako na kitambulisho,
 • Jaza fomu ya maombi kuomba kibali kuzamisha au kupanua kisima /kisima cha kina kirefu,
 • Ada ya maombi ni lazima ilipwe,
 • Baada ya siku 14, kibali hutolewa /kukataliwa,
 • Baada ya kupewa kibali:
  • Tembelea ofisi za wakala ya uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa iliyokaribu yako
  • Jiandikishe
  • Utafiti wa haidrolojia utafanywa kwenye eneo
  • Utapewa ripoti kuhusu kina cha kisima
  • Uchimbaji na ujenzi wa kisima cha kina kirefu
  • Kufanya majaribio ya pampu

Gharama za Ujenzi

 • Mzingo wa kina cha kisima/kisima cha kina kirefu, mabomba vitakavyotumiwa katika ujenzi.
 • Umbali baina ya eneo la ujenzi wa kisima na ofisi
 • Kupatikana kwa eneo la ujenzi wa kisima
 • Gharama za usimamizi
 • Gharama za kukodi zana.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page