Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba Vibali
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Maji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Ili rasilimali ya maji iwe endelevu lazima kuwepo na utaratibu maalum ambao utasaidia katika kuilinda rasilimali hii kwa ustawi wa jamii na mazingira. Maji hutumika katika shughuli mbalimbali mfano za kibiashara (mfano makampuni ya kutengeneza maji ya kunywa, biashara ya kusambaza maji (maboza), kwa walionunua ardhi yenye chanzo cha maji juu ya ardhi). Vyanzo vyote vya maji pamoja na matumizi yote ya maji lazima ya sajiliwe katika mamlaka husika.  

 TARATIBU

  • Fika katika ofisi ya bonde la maji iliyoko karibu nawe, ukiwa na kitambulisho
  • Jaza fomu ya maombi ili kupata kibali cha kutumia maji
  • Utaambatanisha na Ada(ambazo hutofautiana kutokana na aina ya matumizi ya maji)
  • Ombi hutangazwa kwenye gazeti la serikali na tangazo hilo kuwekwa kwenye mbao za matangazo kwa wakuu wa wilaya husika
  • Ofisi ya bondeitaomba maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kama kutakuwa na athari endapo mwombaji atapewa hati ya kutumia maji kutoka chanzo cha maji husika
  • Baada ya siku 40 kupita tangu kuombwa kwa maoni, ombi linaweza kufikishwa katika kikao cha bodi ya maji ya bonde
  • Hati hutolewa kwa maombi yaliyoidhinishwa na kikao cha bodi

GHARAMA

  • Ada ya kuomba kibali
  • Ada ya matumizi ya maji kwa mwaka
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page