Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba Uraia
OFISI INAYOHUSIKA
Uhamiaji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Mtu yeyote ambaye siyo raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzaliwaau kurithi anaweza kuomba uraia wa Tanzania kwa Tajnisi kwa mujibu wa vifungu Na. 8, na 9(1) vya Sheria ua Uraia ya 1995.

Kwa mujibu wa sheria hiyo Mhe. Waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya uraia nchini (kwa sasa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi) ndiye mwenye mamlaka ya mwisho kutoa au kutotoa uraia wa Tanzania kwa wageni walioomba uraia.

 

Masharti:

 • Mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi na awe na uwezo wa kufanya maamuzi yanayokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi.
 • Awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miezi  12 mfululizo kabla ya kutuma maombi.
 • Katika muda wa miaka kumi kabla ya miezi kumi na miwili hiyo awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda usiopungua miaka saba.
 • Awe anaelewa vizuri lugha ya Kiswahili au kiingereza
 • Awe na tabia nzuri
 • Awe alichangia na ataendelea kuchangia katika ukuzaji uchumi, sayansi na teknolojia  na utamaduni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 • Awe anakusudia kuishi moja kwa moja ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ombi lake la uraia litakubaliwa.

 

Taratibu:

 • Mwombaji anatakiwa kujaza fomu za maombi (Fomu A)
 • Wasilisha kwa Katibu Mtendaji wa kata au sheha kwa upande wa Zanzibar.
 • Maombi yatawasilishwa kwa ofisa uhamiaji wa Wilaya.
 • Lipa ada iliyoelezwa ya Dola za marekani 1500 isiyorudishwa.
 • Atangaze kwenye matoleo mawili mfululizo ya magazeti ya kila siku yaliyosajiliwa Tanzania ya kuomba uraia wa kuandikishwa.
 • Atahojiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.
 • Ofisa uhamiaji wa wilaya anapeleka maombi kwa ofisa uhamiaji wa mkoa halafu kwenye kamati ya ulinzi usalama ya mkoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
 • Afisa uhamiaji wa mkoa anapeleka maombi kwa Kamishna Mkuu wa uhamiaji kwa ajili ya mapendekezo yake kwa waziri.
 • Huko Zanzibar kabla maombi kupelekwa kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar atapeleka maombi ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya mapendekezo na

baadaye kuwasilishwa kwa kamishina mkuu wa uhamiaji kwa ajili ya mapendekezo

kwa waziri.

 • Kamishna mkuu wa Uhamiaji anapeleka maombi yaliyopendekezwa kwa waziri.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page