Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Dhima ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), ilivyofafanuliwa kwenye Sheria ya Vyuo Vikuu 2005, ni pamoja na kutambua, kusajili, utambuzi rasmi na usimamizi wa ubora wa vyuo vya umma na vya binafsi vya elimu ya juu nchini Tanzania, programu zao, kozi, wanafunzi, walimu na tuzo. Miongoni mwa mambo mengine, TCU inaratibu udahili wa wanafunzi kwenye programu mbalimbali za shahada ya kwanza kwa vyuo vikuu nchini Tanzania.

Masharti:

Udahili wa waombaji kwenye taasisi za elimu ya juu hufanywa kupitia Mfumo Mkuu wa Udahili unaoruhusu makundi yafuatayo kuomba:

i. Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita

ii Elimu ya Ufundi Ngazi ya Sita (NTA6)

iii. Cheti cha Ualimu wa Ufundi Sadifu (FTC)

Waombaji wenye Vyeti vya Nje ya Nchi

Taratibu

i. Fungua tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz)

ii Fungua Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwenye tovuti kuthibitisha kuwa una sifa zinazostahili kwa ajili ya programu uliyoomba.

iii. Bofya “CAS” kwenye menyu ya juu ya tovuti ya TCU ili kufungua Mfumo Mkuu wa Udahili.

iv. Bofya kitufe cha Usajili.

v. Chagua kundi lako (k.m. kidato cha Sita au Nchi za Nje).

vi. Jaza fomu ya usajili kwa ukamilifu.

vii. Baada ya kujaza fomu, bofya kitufe cha Sajili

viii. Ujumbe utaoneshwa na jina lako la mtumiaji kukuarifu kuwa umefanikiwa kusajiliwa.

ix. Ingia kwenye wasifu wako kwa kutumia jina la mtumiaji.

x. Ingiza nywila yako (ile uliyoitengeneza wakati wa usajili).

xi. Bofya Ingia.

xii. Bofya kitufe cha Maombi.

xiii.Chagua PROGRAMU MOJA TU kutoka vyuo vikuu ambavyo bado vina nafasi.

xiv.Bofya visanduku vya uthibitisho hapo chini.

xv.Wasilisha maombi yako.  

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 25-01-2017
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page