Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kusafirisha/Kuingiza
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Masharti /Taratibu:

 • Wakala wa meli  anatayarisha na kuingiza Hati ya usafirishaji kwa meli kwa kutumia mtandao na kuipeleka Idara ya Forodha ya TRA na Wakala wa Upokeaji na Usafirishaji Mizigo (CFA) aliyeteuliwa.
 • CFA anapata Hati ya Utoaji ya Idara ya Forodha (CRO) kutoka TRA na kuwasilisha Hati ya Usafirishaji wa meli na CRO kwa TPA.
 • Ankara inatolewa kwa ajili ya malipo ya gharama za Bandari kupitia benki.
 • TPA  inahakiki  malipo kwenye mfumo wa benki.
 • Ofisi ya mapato ya TPA inatoa stakabadhi AU inakataa iwapo kuna dosari zozote na CFA inashauriwa  ipasavyo.
 • CFA aingiza Hati ya taarifa za lori (TAD) kwenye mfumo wa mizigo.
 • TAD  ni lazima ionyeshe namba ya usajili wa lori, sehemu ya uwasilishaji, jina la dereva wa lori na namba ya leseni yake.
 • Dereva anapata tiketi ya kuingia kutoka idara ya biashara , mfumo wa mizigo.
 • Ofisa wa TPA anapokea nakala ya tiketi ya kuingia kutoka kwa dereva wa lori na CFA.
 • Anahakikisha na kulinganisha taarifa za mfumo wa mizigo.
 • TPA inakubali mizigo kwa ajili ya kusafirisha kwa meli.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 24-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page