Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kusafirisha/Kuingiza
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Taratibu/Masharti

 • Wakala wa meli (SA) aingiza orodha ya bidhaa kwenye mfumo wa mizigo.
 • SA anatayarisha hati ya uwasilishaji  (DO) na kuingiza kwenye mfumo wa mizigo kupitia tovuti ya TPA.
 • Wakala wa upokeaji na usafirihaji mizigo (CFA)anapata DO (nakala iliyochapwa).
 • CFA anapata Hati ya Idara ya Forodha (CRO) kutoka TRA.
 • CFA anawasilisha DO na CRO kwenye ofisi ya mapato ya TPA.

Ofisi ya mapato ya TPA

 • Inapokea DO (makala iliyochapwa) kutoka kwa SA.
 • Inalinganisha DO na orodha ya Bidhaa kwenye Mfumo wa Mizigo.
 • Thamani ya mizigo ya TRA (c.i.f) inaingizwa kwenye mfumo  wa mizigo wa TPA kwa kulinganisha na mfumo wa TRA ASYCUDA.
 • TPA inahakikisha uhalali wa DO na CRO zilizowasilishwa na CFA.
 • TPA inatoa ankara kwa gharama za bandari.

Ofisi ya mapato ya TPA

 • Inahakiki malipo kwenye mfumo wa Benki.
 • Inatoa stakabadhi ya mapato  AU inakataa iwapo kuna dosari zozote na kurekebisha mfumo wa mizigo.
 • CFA anaingiza Hati ya taarifa za Lori (TAD) kwenye mfumo wa mizigo.
 • TAD ni lazima ionyeshe namba ya usajili wa lori, sehemu ya uwasilishaji, jina la dereva wa lori na namba ya leseni yake.
 • Dereva anapata tiketi ya kuingia kutoka idara ya biashara, mfumo wa mizigo.
 • Kwa lori lililopakia mizigo, dereva atapata kibali cha kuingia lango A kutoka ofisi ya kuwasilisha mizigo.
 • CFA na dereva wa lori wanawasilisha TAD (nakala iliyochapwa) kwenye Lango la TPA
 • CFA na dereva wa lori wanawasilishwa nakala ya kibali cha kuingia lango A mahali pa ukaguzi katika idara ya biashara kwa ulinganishaji kwenye mfumo wa mizigo.
 • Walinzi wanahakiki kibali cha kuingia kwenye mfumo wa mizigo.
 • Iwapo ni sahihi, wanairuhusu lori kutoka.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 25-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page