Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Nishati na Madini

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Wizara ya Nishati na Madini (MEM) uendelezaji wa nishati na madini kupitia ushirika wa wadau mbalimbali wakiwemo wa serikali, binafsi na ubia  wa sekta binafsi na serikali, wananchi, AZISE na vyama vya kiraia. Utoaji wa leseni za haki za madini ni miongoni mwa huduma zinazotolewa na Wizara. Sehemu ya usimamizi wa utoaji leseni na haki za madini na Ofisi za Kanda za migodi zina wajibu wa kupokea na kushughulikia maombi ya haki za madini, kutayarisha taratibu za utoaji leseni na haki za madini, ufuatiliaji wa ufuasi  wa sheria ya uchimbaji madini wa wenye leseni,  kutayarisha taarifa za utoaji leseni kwa matumizi ya umma na ushughulikiaji ya malalamiko yanayohusu utoaji wa leseni.

Masharti:

Waombaji wa Haki za Madini (Leseni za Utafutaji, aina zote za leseni za madini,) ni lazima wahakikishe yafuatayo:

Kustahili kuomba leseni mahususi kunajumuisha :

  • Umri wa zaidi ya miaka 18
  • Leseni za uchimbaji madini mdogomdogo na leseni za uchimbaji wa mawe ya vito kwa wananchi tu; na
  • Uwezeshaji wa kiufundi na kifedha kadiri inavyotakiwa na leseni husika.

Taratibu:

Peleka maombi kwa mamlaka ya utoaji Leseni inayohusika kwa wakati kwa sababu haki za madini zinatolewa kwa ushindani kwa kanuni ya anayeomba kwanza ndiye anayehudumiwa kwanza. Zingatia  kuwa:

  • Maombi ya leseni zautafutaji na leseni za uchakataji zinzpokewa katika ofisi yan kamishna wa madini, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
  • Maombi ya leseni ya uchimbaji madini maalum, leseni ya uchimbaji madini, leseni ya ubakizaji, leseni ya uyeyushaji, leseni ya usafishaji, zinzpokewa katika Ofisi ya Waziri, Makao Makuu.
  • Maombi ya uchimbaji madini mdogomdogo,leseni ya muuzaji, na leseni ya dalali zinapokelewa kwenye ofisi za mgodi za kanda husika  zilizopo Dar es Salaam (UN Road), Arusha, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Singida, na Mpanda.

Saa za kazi za ofisi ni kuanzia saa 1:00 mpaka 9:00 Jumatatu hadi Ijumaa.

Hakikisha kuwa maombi ni sahii na kamili kabla ya kuwasilisha.  Tumia fomu inayohusika kulingana na leseni iliyoombwa na ambatanisha nyaraka sahihi. Viambatanisho muhimu ni:

  • Picha tatu za pasipoti za hivi karibuni kwa mwombaji binafsi;
  • Maombi ya leseni ya uchimbaji madini mdogomdogo ni lazima yaambatanishwa na ramani ya eneo lililoombwa  na mipaka ya kijiografia ya eneo lililoombwa katika ramani ya taarifa na takwimu za Arc 1960. Maombi kwa ajili ya maeneo ya pekee kwa ajili ya wachimbaji madini wadogowadogo yanaweza kuwa na masharti ya nyongeza ambayo lazima yatimizwe.
  • Waombaji wa shirika/kampuni ni lazima waambatishe ramani ya mandhari (topografia) na mipaka ya kijiografia ya eneo lililoombwa kwenye ramani ya taarifa na takwimu Arc 1960, cheti cha Usajili, Katiba ya Kampuni, maelezo mafupi yanayoonyesha uwezo wa fedha  na wa kiyfundi,  mpango wa mafunzo  na mpango wa kununua bidhaa za nchini.

Tuma kiasi sahihi cha ada ya maombi wakati wa maombi. Ada zote za haki za madini hazitarudishwa.

Zingatia: Malipo yote yatalipwa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya  Nishati na Madini.  Pata maelekezo ya malipo kutoka kwa wafanyakazi wa utoaji wa leseni kwenye ofisi husika.

Maelezo zaidi yanapatikana kwenye ofisi za migodi na ramani za utoaji wa leseni za umiliki zinaweza kuangaliwa kwenye tovuti: www.flexicadastre.com/tanzania

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 25-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page