Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

“Huduma za Maudhui” maana yake ni huduma zinazotolewa za sauti, data, maandishi au picha, ziwe za mnato au zinazotembea, isipokuwa kama zimerushwa kwenye mawasiliano binafsi.

 Masharti:

 • Kupokea ada ya maombi
 • Mpango wa biashara
 • Mpango wa kuanza kutumia mtandao
 • Usajili wa Kampuni/Cheti cha Usajili 
 • Taarifa kuhusu pendekezo la kiufundi la huduma itakayotolewa
 • Taarifa ya uzoefu
 • Wasifu wa kampuni
 • Uthibitisho wa uwezo wa kifedha

Taratibu:

 • Kujaza fomu ya maombi kwa ukamilifu
 • Kuwasilisha fomu iliyojazwa
 •  Kuweka maombi kwa makundi
 • Kutathmini iwapo maombi yana viambatisho vyote vinavyohitajika
 • Kufanya tathmini ya kina ya maombi kwa kuzingatia  vigezo vilivyowekwa
 • Kutoa tangazo la orodha ya waombaji kwenye magazeti na kuwekwa kwenye tovuti ya Mamlaka ili kutaka maoni ya wananchi
 • Timu ya tathmini kupitia maoni ya wananchi
 • Kualika waombaji kujieleza
 • Mapendekezo ya timu ya tathmini kupelekwa Menejimenti kwa kutoa uamuzi
 • Mapendekezo ya Menejimenti yatawasilishwa kwenye Bodi kwa idhini
 • Maombi yaliyoidhinishwa na Bodi yatawasilishwa kwa Waziri kwa ushauri
 • Kulipa ada inayostahili (ada ya mwanzo, ada ya mtumiaji masafa, utiaji namba n.k.
 • Leseni kutolewa kwa waombaji waliofanikiwa

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 22-12-2016
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page