Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba Vibali
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Kazi na Ajira

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Kibali cha kufanya kazi ni idhini anayopewa mgeni kuingia nchini kwa madhumuni ya kufanya biashara au kwa wale wenye taaluma inayohitajika. Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira ya Wasio Raia ya Mwaka 2015(1) kibali cha kufanya kazi kitatolewa na Kamishina wa Kazi.

Vibali hutolewa katika daraja  tano:

Daraja A, inahusisha wawekezaji na waliojiajiri.

Daraja B, inahusu raia mwenye taaluma inayotambulika,

Daraja C, inatolewa kwa wasio raia wenye taaluma nyingine,

Daraja D, inatolewa kwa wasio raia walioajiriwa au wanaofanya kazi katika taasisi za dini zilizosajiliwa au huduma za msaada,

Daraja E, inatolewa kwa wakimbizi.

MASHARTI YA KIBALI CHA KUFANYA KAZI DARAJA A

 • Barua ya Uthibitisho;
 • Jaza Fomu ya Maombi TFN 901 (Fomu 2);
 • Picha mbili za hivi karibuni za mwombaji zikiwa kwenye MANDHARI YA BLUE,
 • Fotokopi ya pasipoti inayotumika;
 • Idhini ya sekta inayohusika (pale inapohitajika);
 • Kibali cha kufanyakazi cha zamani (kwa maombi ya kuongeza muda); leseni ya kiwanda/biashara/leseni inayotumika kwa kazi inayohusika;
 • Cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN);
 • Cheti cha Kodi ya Ongezeko la Thamani – VAT (pale inapohitajika);
 • Cheti cha Usajili wa Biashara/jina la biashara;
 • Sehemu ya Katiba ya Kampuni kutoka kwa   Msajili wa Kampuni/Katiba/hati yoyote nyingine ya kisheria, na
 • Cheti cha Motisha (kama kipo).

Masharti ya Kibali cha Kufanya Kazi Daraja B, C na D

 • Barua ya Uthibitisho (Barua ya maelezo ya ziada);
 • Fomu ya Maombi TFN 901 (Fomu 2);
 • Mkataba wa Ajira kutegemea aina ya ajira uliotiwa saini kwa ukamilifu na pande zote zinazohusika;
 • Ainisho la kazi;
 • Wasifu;
 • Picha mbili za hivi karibuni za pasipoti za mwombaji;
 • Cheti cha Utambuzi rasmi, kama kipo kutoka vyombo vya kitaaluma vinavyotambuliwa; vyeti vya kitaalam/kitaaluma;
 • Tafsiri iliyothibitishwa ya hivyo vyeti na hati na mamlaka yenye weledi au ubalozi au ofisi ya ubalozi mdogo (iwapo vipo kwenye lugha isiyo ya kiingereza) na nakala ya kibali cha kazi cha zamani (kwa maombi ya kuongeza muda);
 • Leseni za kiwanda/biashara/inayotumika kwa kazi inayohusika;
 • Cheti cha usajili, Jina la Biashara na sehemu kutoka kwa Msajili wa Kampuni;
 • Katiba ya Kampuni;
 • Mpango wa Kurithiana (kwa kuongeza muda);
 • Barua isiyo na kipingamizi (kama ipo) kutoka kwa mwajiri wa zamani;
 • Uthibitisho wa sekta inayohusika (pale inapohitajika), na
 • Cheti cha Motisha (kama kipo).

TARATIBU

 1. Jaza Fomu ya Maombi Na. TFN 901
 2. Lipa ada stahiki kulingana na daraja unayoomba ilivyofafanuliwa hapa chini:

a)      Daraja A $ 1000

b)      Daraja B  $ 500

c)       Daraja C   $ 1000

d)      Daraja E  Gratis

Lipa ada yako Benki ya CRDB kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira, Akaunti Na. 025021174540

ZINGATIA

FOMU ZA MAOMBI YA KIBALI CHA KUFANYA KAZI NA. TFN 901, TFN 903 ZINAPATIKANA KWENYE : www.kazi.go.tz

NYARAKA ZOTE ZINAZOAMBATISHWA NA FOMU ZA MAOMBI  NI LAZIMA ZITHIBITISHWE.

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 28-01-2016
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page