Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kutoa Malalamiko
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari-MAELEZO inaratibu na kusimamia Tovuti Rasmi ya Wananchi ambayo humuwezesha mwananchi kuwasilisha maoni, malalamiko (Hoja) Serikalini kupitia mtandao wa intaneti, ujumbe wa simu ya mkononi , barua kwa Mkurugenzi, Idara ya Habari (MAELEZO) S.L.P 8031, Dar es Salaam au kufika ofisi za Idara.

Taratibu:

  • Jaza Fomu ya Usajili wa Hoja kutuma hoja kwa njia ya intaneti. Au
  • Tuma ujumbe mfupi wa maandishi kwenda Namba 1500. Au
  • Tuma barua kwa Mkurugenzi, Idara ya Habari-MAELEZO, S.L.P 8031, Dar es Salaam. Au
  • Tembelea Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO zilizopo Mtaa wa Samora mkabala na Benki ya NMB tawi la Benki House na kuonana na Afisa Habari na kueleza hoja yako.

 

Zingatia:

  • Kuhifadhi namba yako ya usajili wa tiketi (TRN) yako ili uweze kufuatilia majibu ya hoja yako.
  • Epuka kutumia lugha isiyo ya staha
  • Hakikisha hoja yako inaeleweka na ambatisha nyaraka muhimu ili kurahisha majibu ya hoja yako.
  • Epuka kutuma hoja isiyohusu Serikali au Taasisi ya Serikali.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 26-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page