Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Kabla ya usajili, mwombaji lazima apate kibali cha uhamisho wa Haki Miliki kutoka kwa kamishna wa ardhi au afisa Ardhi mteule wa manispaa husika.

 Masharti ya kupata kibali cha Kamishna au afisa ardhi mteule

(a)Awe na Hati miliki

(b)Hati za uhamisho zenye picha ya muuzaji na mnunuzi (Transfer Deed)

(c)Hati ya mauziano yenye picha ya muuzaji na mnunuzi (Sale Agreement)

(d)Nakala halisi ya cheti cha usajili wa kampuni kama mnunuzi ni kampuni

(e)Taarifa ya uhamisho kwa Kamishna wa Ardhi (Land Form No.30)

(f)Risiti za malipo ya kodi ya ardhi

(g)Risiti za malipo ya ushuru na ada ya usajili

(h)Taarifa ya uthamini

(i)Uthibitisho wa uraia

 Utaratibu

Wasilisha taarifa zote hapo juu kwa Kamishna wa Ardhi, au Afisa ardhi mteule kwa ajili ya kupatiwa Cheti cha kibali cha uhamisho wa milki (Form No.33).  Baada ya kupata kibali cha uhamishaji, peleka nyaraka zote hapo juu ofisi ya TRA kwa ajili ya kupatiwa  Cheti cha malipo ya kodi ya mapato (Capital Gain Tax Clearence Certificate)

Zingatia

Kama nyaraka zote zimekamilika na ziko sahihi, hakikisha unazipeleka katika ofisi ya msajili wa hati kwa ajili ya usajili kama kiwanja husika kilikuwa na Hati miliki. Endapo hati miliki ilikuwa bado haijaandaliwa, peleka taarifa zote hapo juu ofisi ya Halmashauri husika kwa ajili ya kuandaliwa hati miliki

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 26-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page