Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Mwananchi anaweza kutumia Haki yake ya umiliki wa kiwanja (Title Deed) kama chanzo cha mapato kwa kuiweka rehani na kuomba mkopo katika taasisi yeyote ya kifedha.

 Masharti ya kupewa usajili wa mkopo

(a)Awe na Hati miliki

(b)Hati ya rehani (Nakala 2 au zaidi)

(c)Hati ya kutoa taarifa kw Kamishna wa ardhi (Notification of Disposition)

(d)Risiti za malipo ya kodi ya ardhi

(e)Kibali cha mke/mume au kiapo (spouse consent or affidavit)

(f)Taarifa ya uthamini

(g)Nakala halisi ya cheti cha usajili wa kampuni kutoka kwa msajili wa makampuni ikiwa mkopaji ni kampuni

Utaratibu

(a)Hakikisha una nyaraka zote tajwa hapo juu

(b)Wasilisha nyaraka hizo ofisi ya msajili wa hati kwa ajili ya usajili wa mkopo

(c)Nyaraka za usajili zitakuwa tayari ndani ya siku 14 za kazi

(d)Chukua nyaraka zilizosajiliwa(ofisi ya msajili wa hati) na peleka katika taasisi uliyoomba mkopo.

Zingatia

Ukisharejesha deni ulilokopa kwa kuweka reheni hati miliki yako, hakikisha unaomba kufuta usajili wa mkopo ili urudishiwe hati miliki yako na taasisi husika.

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 28-01-2016
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page