Visitors Feedback Form


   | 
United Republic of Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Sheikh Abeid Amani Karume
How Do I
Read More » ...
 
 
Home HOW DO I Apply
GOVERNMENT OFFICE RESPONSIBLE
Nationa Social Security Fund - NSSF

RATING
Usefulness
()
Ease of Access
()
 

Utaratibu wa kuomba mafao ya NSSF ni kama ufuatavyo;

Mafao ya Uzee

Fika ofisi ya NSSF ukiwa na Barua ya kustaafu kutoka kwa mwajiri, kadi yako ya uanachama ya NSSF na kopi yake, picha tatu za paspot saiz na kopi ya kadi ya benki.

Utapatiwa fomu NSSF/R.6 NA NSSF/B.1 ujaze  kisha utafunguliwa madai

 

Mafao ya Ulemavu

Fika ofisi ya NSSF ukiwa na ripoti kuhusu ulemavu kutoka kwa jopo la madaktari,kadi ya uanachama ya NSSF na kopi yake pamoja na picha tatu za paspot saiz.

Utapatiwa fomu NSSF/B.1 ujaze  kisha utafunguliwa madai

 

Mafao ya Urithi

Fika ofisi ya NSSF ukiwa na viambatanisho vifuatavyo;

.Cheti cha kifo,  kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama

.Muhtasari wa kikao cha wanandugu, kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama

.Cheti cha ndoa ikiwa mafao yatafunguliwa na mwenza wa marehemu, kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama

.Cheti cha kuzaliwa ikiwa madai yatafunguliwa na mtoto wa marehemu, kopi yake iwe imethibitishwa na mahakama

.Fomu namba 4 ya usimamizi wa mirathi ambayo hutolewa na mahakama

.Kadi ya uanachama ya NSSF kama ipo na kopi yake

Utapatiwa fomu NSSF/B.2 na NSSF/ B.18 ujaze  kisha utafunguliwa madai

 

Mafao ya Uzazi

Mwanachama anatakiwa kufungua madai akiwa wiki ya 24 ya ujauzito au ndani ya siku 90 baada ya kujifungua

Fika ofisi ya NSSF ukiwa na picha tatu za paspot saiz, kadi ya uanachama ya NSSF na kopi yake pamoja na kopi ya kadi ya benki.

Utapatiwa fomu MB1,MB2 na MB3  kisha kufunguliwa madai

 

Msaada wa mazishi

Fika ofisi ya NSSF ukiwa na Kibali cha mazishi/cheti cha kiufo,risiti halisi ya gharama za mazishi zinazomuhusu marehemu moja kwa moja, muhtasari wa kikao cha wanandugu kumteua anayekuja kufungua madai haya pamoja na kadi ya marehemu ya uanachama wa NSSF kama ipo.

Utapatiwa fomu NSSF/B.3 ujaze kisha utafunguliwa madai.

 

Mafao ya Matibabu (SHIB)

Fika ofisi ya NSSF ukiwa na vyeti vya kuzaliwa vya watoto (nakala halisi na kopi mbili kwa kila cheti) kwa mwanachama mwenye mtoto, Cheti cha ndoa kwa mwanachama mwenye mwenza (nakala halisi na kopi mbili), picha tatu za paspot saiz kwa mwanachama na tatu kwa kila mtegemezi.

Utapatiwa fomu SHIB 3A ujaze na Kuandikishwa kwaajili ya mafao ya matibabu.

 

Kurudishiwa michango ya Uanachama/Kujitoa

Fika ofisi ya NSSF ukiwa na nakala halisi na kopi ya barua ya kuacha kazi kutoka kwa mwajiri, Kadi ya uanachama ya NSSF na kopi yake, picha tatu paspoy saix na kopi ya kadi ya benki.

Utapatiwa fomu NSSF B.17 ujaze na NSSF/R.6 upeleke kwa mwajiri kisha utafunguliwa madai

Source: Government Portal Content Team, Last Reviewed on: 29-10-2018
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page