Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Nishati na Madini

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Tanzania imebarikiwa kuwa na hazina kubwa ya rasilimali ya madini, kama vile dhahabu, almasi, vito , nikeli, urani, makaa ya mawe, jasi, chumvi na kadhalika. Hazina yote ya madini inamilikiwa na Serikali, na hivyo shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini huweza kufanywa na watu au kampuni kwa kutumia leseni zinazotolewa na Wizara ya nishati na Madini.

Madaraja ya leseni ya uchimbaji madini yako kama ifuatavyo;

 • Daraja A: Leseni za Utafutaji Mkubwa wa Madini-PL
 • Daraja B:Leseni za Uchimbaji wa Madini
 • Daraja C: Leseni za Uchimbaji Mdogo wa Madini-PML
 • Daraja D: Leseni za Uchenjuaji wa Madini

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUOMBA LESENI

Kabla ya kujaza fomu ya kuomba leseni ni muhimu kufanya maandalizi ya vitu muhimu vifuatavyo;

 • Kupata taarifa za uhakika kuhusu eneo unalotaka kuomba. Ofisi zote za madini huweza taarifa zinazohitajika
  kwa maombi maalum (official search). Aidha, wateja wanaweza kununua ramani ya leseni ya madini (shapefile)
  inayopatikana kwa kuwasilisha ombi Makao Makuu ya Wizara. Ramani ya jumla inapatikana kwenye tovuti ifuatayo: www.flexicadastre.com/tanzania
 • Kwa waombaji kupitia kampuni wanapaswa kuandaa nyaraka sahihi za usajili wa kampuni (Certificate of Incorporation, Memorandum & Articles of Association) pamoja na nyaraka zinazoonesha uwezo wa kifedha na kiufundi (financial & technical capability) Waombaji binafsi wanatakiwa kuandaa picha tatu za pasipoti na kama ni kikundi, basi picha za wanakikundi wote ziandaliwe.
 • Waombaji wa leseni za madaraja A na B wanapaswa kuandaa ramani ya eneo linaloombwa (topographical map), kuchukua vipimo vya kijiografia vya eneo linaloombwa (geographical coordinates in Arc 1960); na kutayarisha mpango wa kazi unaoonesha mpango wa mafunzo(training plan) na mpango wa manunuzi ya bidhaa (procurement of local goods).
 • Waombaji wa leseni za uchimbaji mdogo wanapaswa kuandaa mchoro unaoonesha mahali panapoombwa na pia kuchukua vipimo vya kijiografia vya eneo linaloombwa (geographical coordinates in Arc 1960). Waombaji kwenye maeneo yaliyotengwa rasmi kwa uchimbaji mdogo wanaweza kutakiwa kuwasilisha maelezo au vitu zaidi kadiri itakavyotakiwa na Kamati ya Ugawaji.
 • Waombaji wanapaswa kutayarisha fedha za kulipia ada ya maombi (application fee) wakati wa kuwasilisha fomu ya maombi. Ada ya maombihairejeshwi hata kama ombi husika litakataliwa.
 • Ni MUHIMU kuwahisha ombi lililokamilika mapema na kulipia katika ofisi ya madini inayosimamia eneo unaloomba.
 • Taratibu za kuomba vibali toka mamlaka nyingine (vijiji, maliasili nk) ni WAJIBU wa Mteja. Ni muhimu Wateja wakafahamu masharti
  ya kupata vibali toka mamlaka husika katika maeneo wanayotaka kuomba leseni ili kuepuka usumbufu haitakiwi kuweka mipaka au kutengeneza miundombinu kabla hujapata leseni na pia kabla hujapata ridhaa ya wenye kumiliki eneo unaloomba leseni

 Kwa maelezo zaidi ya kujua utaratibu huu wa kupata leseni ya uchimbaji wa madini bofya hapa.

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 28-01-2016
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page