Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Taasisi ya Uendelezaji na Usimamizi wa Maji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Utangulizi: Chuo cha Maji (WI) ni Wakala ya utendaji ya serikali katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji iliyoanzishwa kukidhi mahitaji ya wataalam wa maji

Tunawakaribisha wanafunzi wote wanaotaka kujiunga kwa masomo ya muda mrefu na muda mfupi kwenye nyanja zozote za maendeleo ya maji (huduma za maji) na usimamizi wa rasilimali za maji kutoka Tanzania, Afrika Mashariki, Nchi zinazoambaa Mto Nile, Nchi za SADC na nchi nyingine za ndani na nje ya Bara la Afrika. Pia tunawakaribisha watu na mashirika yanayohitaji huduma za ushauri na uelekezi katika uendelezaji wa maji (huduma za maji) na usimamizi wa rasilimali za maji kuwasilisha mahitaji yao katika Chuo ili tuweze kuandaa taratibu za kuwahudumia.

 Masharti:

Shahada ya Kwanza ya Miaka Minne ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji

 • Kiwango cha chini cha sifa ya udahili kujiunga na Shahada ya Kwanza ni Diploma ya Juu katika  Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji.
 • Cheti cha Kuzaliwa.
 • Vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari na au Kidato cha Sita
 • Diploma ya Kawaida ya Uhandisi  katika Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingira, Haidrolojia na Uchimbaji wa Visima, Haidrolojia na Utabiri wa Hali ya Hewa, Teknolojia ya Maabara ya Maji, Uhandisi Ujenzi, Uhandisi wa Umwagiliaji na nyanja nyingine zinazohusiana na Uhandisi Ujenzi au Uhandisi wa Rasilimali za Maji yenye  jumla ya alama za Ufaulu 2.7

Diploma ya Kawaida ya Miaka Mitatu

                                                                 

 • Cheti kamili cha Ufundi (FTC) katika Uhandisi wa Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingira
 • Haidrojiolojia na Uchimbaji Visima, Haidrolojia na Utabiri wa Hali ya Hewa, Teknoloji ya Maabara ya Maji, Uhandisi Ujenzi, Uhandisi wa Umwagiliaji na nyanja nyingine zinazohusiana  na Uhandisi Ujenzi au Uhandisi wa Rasilimali za Maji chenye ufaulu wa wastani wa Alama 3.0 kwa ulinganishi wa: A=5; B=4; C=3, D=2
  Cheti cha Kidato cha Sita (ACSE) chenye ufaulu wa somo kuu katika Hisabati na Fizikia na ufaulu wa somo dogo katika Kemia au Jiografia yenye jumla ya Alama 3.5 kwa ulinganishi wa: A=5, B=4, 
  C=3, D=2, E=1, S=0.5 na F=0

 

Cheti cha Mwaka Mmoja:

 • Masharti ya programu yoyote ya Cheti ni sawa na programu za diploma.
 • Muda wa masomo ya Cheti ni mwaka mmoja wa masomo

 

Taratibu:                                     

 •  Pakua fomu ya maombi kutoka kwenye tovuti ya Chuo.
 • Ada ya maombi ni lazima ilipwe kupitia Benki.
 • Viambatisho vyote vikiwemo vyeti vya masomo na hati ya kulipia Benki ni lazima viambatishwe pamoja na fomu za maombi.
 • Fomu ya maombi iliyojazwa kwa ukamilifu ni lazima irudishwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Chuo, Jengo la Utawala, Kampasi ya Chuo Ubungo, Barabara ya Chuo Kikuu, kuchepuka Barabara ya Sam Nujoma, 

Dar es salaam.

 • Angalia tarehe ya mwisho ya maombi kwenye tovuti ya Chuo.

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 22-12-2016
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page