Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kutoa Malalamiko
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Uthibiti wa Nishati na Maji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

EWURA inashughulikia malalamiko dhidi ya watoa huduma   au  bidhaa zilizo chini ya mamlaka yao kwa jambo lolote linalohusu  utoaji  au utoaji unaotarajiwa au unaopendekezwa wa huduma au bidhaa. Kuna kitengo maalum kilichoko kwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kinachopokea na kufuatilia malalamiko kutoka kwa watumiaji wa bidhaa au huduma zinazosimamiwa na Mamlaka. Kitengo hicho kilianzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 34 cha Sheria ya EWURA SURA 414 kinachofahamika kama Huduma kwa Mteja.

Sera ya utaratibu wa kushughulikia malalamiko inahusu:

 • Kumlinda mtumiaji – huwataka watoa huduma kutoa huduma au bidhaa za kuaminika, bora na za bei nafuu;
 • Kupenda utaratibu wa kusuluhisha malalamiko nje ya mahakama  kuliko kukimbilia mahakamani;
 • Kuwa na utaratibu wa kushughulikia malalamiko kwa haraka usio na mizunguko.

Kuwasilisha malalamiko:

 • Mtu yeyote (mtumiaji) anaweza kuwasilisha malalamiko ;
 • UWURA CCC au mwakilishi aliyeidhinishwa;
 • Kikundi cha watu kinaweza kuwasilisha malalamiko kwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo:
  • Orodha ya majina na saini,
  • Kumbukumbu za mkutano na azimio la kuwasilisha malalamiko,
  • Jina/majina ya mwakilishi/wakilishi  na mawasiliano yao.

Malalamiko yawasilishwe katika muda maalum ili kumwezesha mtoa huduma kuwajibika. Malalamiko yatayowasilishwa baada ya muda maalum hayatashughulikiwa na hivyo mlalamikaji atapoteza haki ya huduma bora  au bidhaa. Sababu kuu ya kuweka muda maalum ni kuwezesha Mamlaka kushughulikia  malalamiko kwa wakati na kukusanya ushahidi utakaosuluhisha kwa uadilifu.

Mwezi Januari 2013, Mamlaka  ilitunga Kanuni kuhusu Utaratibu wa Kusuluhisha Malalamiko , GN Na. 10 ya 2013, itakayotumika kushughulikia malalamiko. Muda maalum unazingatia aina ya malalamiko kama ilivyooneshwa hapa chini:

AINA YA LALAMIKO                                                                             UKOMO WA MUDA 

Kukatisha huhuma kinyume cha sheria                                                      Miezi kumi na mbili

Madai yasiyo halali                                                                                    Miezi kumi na mbili

Kushindwa  au kukataa kurudisha huduma                                                Miezi kumi na mbili

Huduma  za kiwango duni                                                                        Miezi ishirini na nne

Mengine                                                                                                  Miezi kumi na mbili

Mamlaka inatoa miongozo kwa watumiaji kuhusu namna ya kupeleka malalamiko, haki na wajibu wa mtumiaji na namna ya kujaza Fomu ya Malalamiko. Mamlaka inatunza Daftari la Malalamiko kwa sekta zote zilizo chini ya Mamlaka.  

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 28-01-2016
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page